Lissu alalamikia matumizi mabaya ya Mahakama, achoshwa na ahirisho la mara kwa mara
Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga , Lissu amedai kwamba kuendelea kwa hatua za kuahirisha kusomwa kwa shauri hilo ni dhihirisho la namna vyombo vya sheria vinavyoweza kutumiwa kisiasa, jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa demokrasia nchini.