Chadema wapinga wananchi wa Ngorongoro kuondolewa kwenye ardhi yao
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimepinga amri ya Serikali iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serikali namba 673 la tarehe 02 Agosti, 2024, ambapo kwa mujibu wa chapisho hilo imewaondoa wananchi wote wa Tarafa ya Ngorongoro kwenye ardhi yao kwa kufuta Kata, Vijiji na Vitongoji vyote vya Tarafa hiyo.