East Africa Politics Tanzania

Miaka saba tangu Lissu ashambuliwe kwa risasi, bado watuhumiwa hawajashikiliwa

Miaka saba imepita tangu Tundu Lissu, mwanasiasa na kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, aliposhambuliwa kwa risasi mnamo tarehe 7 Septemba 2017. Tukio hili lilileta mshtuko mkubwa siyo tu kwa watanzania bali pia kwa jamii ya kimataifa. Tangu tukio hili kutokea, bado upelelezi wa kina haujafanyika na watuhumiwa hawajashikiliwa, hali inayoendelea kutoa maswali mengi kuhusu usalama wa viongozi wa upinzani na uongozi wa kisheria nchini Tanzania.

East Africa Politics Tanzania

Polisi wadaiwa kutumia nguvu ukamatwaji wa viongozi wa Chadema na wafuasi wake.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu Bara kutoka chama cha Chadema bwana Benson Kigaila ni kwamba katika kundi kubwa la watu takribani 500 waliokamatwa na Polisi kati ya siku hizo mbili, wakiwemo viongozi wakuu wa chama hicho ni kwamba Makamu Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu, Katibu Mkuu John Mnyika na Mwenyekiti Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu wameumizwa vibaya kutokana na nguvu iliyotumika kuwakamata.