Samia Peke Yake? Uchaguzi wa Kwanza Tanzania Uliokosa Wapinzani Wakuu
Tanzania inapiga kura leo, Oktoba 29, 2025, katika uchaguzi mkuu unaoonekana kumwendea Rais Samia Suluhu Hassan, anayewania muhula wa pili kupitia CCM. Uchaguzi huu umechochea mjadala mkali kuhusu uhuru wa kisiasa na haki za binadamu, hasa baada ya kuenguliwa kwa wagombea wakuu wa upinzani.