Watanzania wajiandaa kupiga kura kesho
Tume zote mbili INEC kwa Tanzania Bara na ZEC kwa Zanzibar zimeahidi kufanya uchaguzi ulio huru, wa amani na unaozingatia sheria. Mashirika ya kiraia na waangalizi wa kimataifa pia wanatarajiwa kufuatilia mchakato huo unaotazamwa kama kipimo muhimu cha demokrasia nchini.