TANZANIA:Ufadhili kutoka Shirika la Fedha Duniani kusaidia kujenga uchumi.

Shirika la IMF latoa US$567.25 milioni kusaidia katika juhudi za kuinua uchumi wa Tanzania uliodorora kutokana na mlipuko wa UVIKO 19.

0

Shirika la IMF latoa US$567.25 milioni kusaidia katika juhudi za kuinua uchumi wa Tanzania uliodorora kutokana na mlipuko wa UVIKO 19.

Bodi ya Utendaji ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) tarehe 8 Septemba limeidhinisha US $567.25 milioni kama mkopo kwa Tanzania ambapo kiasi cha US $189.08 milioni umetoka kutoka mpango wa Rapid Financing Instrument (RFI)  na fedha zingine ni kutoka mpango wa Rapid Credit Facility (RCF). Fedha hizi zimelenga kulisaida taifa la Tanzania kushughulikia athari zilizotokana na mlipuko wa UVIKO 19 katika sekta ya afya na uchumi.

Mtazamo wa uchumi wa Tanzania umedorora kutokana na athari za UVIKO 19 pamoja na kuanguka kwa utalii baada ya vizuizi vya usafiri, uchumi unaripotiwa kudorora kwa 4.8% na ukuaji wa uchumi unatarajiwa kusalia hapo mwaka 2021.

Mamlaka za Tanzania zimesema zitajitolea kufuata sera za uchumi zinazofaa ili kukabiliana na athari za janga la UVIKO 19, na kutumia fedha hizo kwa uwazi katika kukabiliana na janga hilo. Kati ya mikakati itakayowekwa ni pamoja na kuchapisha ripoti za jinsi rasilimali za RCF na RFI zitakavyotumiwa na kutoa ripoti ya matumizi yote yanayohusiana na janga la UVIKO 19.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted