Mambo mawili yanayoitambulisha Afghanistan; Taliban na Afyuni

Afghanistan ni taifa linaloongoza katika upanzi wa mmea unaojulikana kama afyuni. Hutumika katika utengenezaji wa dawa tofauti za kulevya ikiwemo heroini.

0
Afyuni (Opium poppy)

Afghanistan ni taifa ambalo limegonga vichwa vya habari katika siku za hivi maajuzi baada ya kundi la Taliban kuiteka nchi na kumfurusha Rais Ashraf Ghani.

Taliban imechukua uongozi wa taifa ambalo limekuwa katika vita na Amerika kwa miaka 20. Amerika ilivamia Afghanistan mwaka wa 2001 ili kuibandua Taliban uongozini na kumsaka Osama bin Laden aliyehusika katika mashambulizi ya kigaidi
katika jumba la biashara la World Trade Centre na Pentagon,9 Septemba 2001.

World Trade Centre

Ingawaje Afghanistan inafahamika zaidi kwa kundi la Taliban na madai ya kuhusika katika kuyapa hifadhi makundi ya kigaidi, taifa hilo linafahamika kwa ukulima wa mmea ambao si wa kawaida.

Afghanistan ni taifa linaloongoza katika upandaji wa mmea unaojulikana kama afyuni, hii ni kulingana na Idara ya Umoja wa Mataifa kuhusu Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).Afyuni hutumika katika utengenezaji wa dawa tofauti za kulevya ikiwemo
heroini.

Taliban ilidai kuwa upandaji wa afyuni ulipungua mara ya mwisho walipokuwa uongozini.Mavuno ya zao la afyuni kutoka Afghanistan ni 80% ya mazao yote ya afyuni yanayotoka mataifa mengine duniani.

Utafiti wa UNODC wa 2018 ulikadiria kuwa uzalishaji wa afyuni ulichangia 11% ya uchumi wa Afghanistan.

Kilimo cha afyuni kiliongezeka sana chini ya utawala wa Taliban kutoka hekta 41,000 mwaka wa 1998, hadi zaidi ya 64,000 mwaka wa 2000.Kulingana na UNODC kilimo cha afyuni huajiri takriban watu 12,000.

Asilimia 95 ya dawa ya kulevya aina ya heroini inayopatikana bara Uropa ni ile iliyokuzwa Afghanistan.

Baada ya Taliban kuchukua tena uongozi wa Afghanistan, msemaji wa serikali Zabihullah Mujahid, amesema watahakikisha kuwa kutakuwa hakuna kabisa uzalishaji wa afyuni nchini humo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted