“Nipo tayari kupatanishwa na Rais Uhuru.” Mhe. William Ruto

"Nipo tayari kupatanishwa na Rais Uhuru." Mhe. William Ruto

0
Naibu wa Rais William Ruto

Mwito kutoka kwa makasisi kutaka kuwepo mapatanisho kati ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, kunaonekana kuzaa matunda baada ya Naibu Rais William Ruto kusema yupo tayari kupatanishwa.

Mwezi uliopita, Muungano wa Kitaifa wa Makanisa ya Pentekoste uliitisha kupatanishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto.

Akiitikia mwito wa Muungano wa Makanisa waliomtembelea nyumbani kwake eneo la Karen jijini Nairobi, Bw. Ruto amesema yupo tayari kwa mazungumzo na rais, akiongeza kuwa uhasama kati yake na rais ulichangiwa na watu ambao hawakuwepo walipounda chama cha Jubilee na Rais Kenyatta, akisema kuwa watu hao wanataka kufaidika na jasho la wengine.

Ruto anasema, makubaliano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani mhe. Raila Odinga mwaka 2018, maarufu ‘Handshake’ yalichangia uhasama huo.

Rais Uhuru na Raila Odinga

Chama cha Jubilee chake Uhuru Kenyatta na William Ruto kiliundwa mwaka wa 2016 baada ya kujumuishwa kwa vyama vingine vidogo 11.

Maskofu wa kanisa katoliki wameelezea wasiwasi wao kuwa uhasama kati ya viongozi hao wawili huenda ukasababisha mgogoro wa kisiasa kati ya wafuasi wao hususan Kenya inapoeleka katika uchaguzi Agosti 2022. Maskofu hao 23 walikutana jijini Nairobi chini ya mwavuli wa maaskofu wa katoliki Kenya, 15 Septemba.

Maaskofu wa katoliki

Bw. Ruto amesema yupo tayari kukutana na Rais Kenyatta bila masharti
yoyote.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted