Nyota wa R&B R. Kelly apatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono

Nyota wa muziki kutoka Marekani,Robert Kelly maarufu R.Kelly amepatikana na hatia ya kutumia umaarufu wake katika kuongoza mradi wa unyanyasaji wa ngono dhidi ya wanawake na watoto kwa...

0
R.Kelly

Nyota wa muziki kutoka Marekani,Robert Kelly maarufu R.Kelly amepatikana na hatia ya kutumia umaarufu wake katika kuongoza mradi wa unyanyasaji wa ngono dhidi ya wanawake na watoto kwa takriban miaka 30.

Walalamishi 11, ikiwemo wanawake tisa na wanaume wawili, walieleza mahakama jinsi walivyodhalilishwa kingono na mateso waliyopitia mikononi mwake.

Mahakama imempata na hatia kwa mashtaka yote tisa, ikiwemo shtaka la utapeli linalojumuisha matendo 14 yakiwemo ya usafirishaji binadamu kwa ajili ya ngono, rushwa, utekaji na kuwatumikisha kwa nguvu.

R.Kelly

Majaji walimpata msanii huyo maarufu kwa nyimbo kama ‘I believe I can fly’ na ‘The world’s greatest” kuwa kiongozi wa mpango uliowavutia wanawake, wavualana na watoto na hatimaye kuwanyanyasa kingono.

Kati ya wanawake waliothirika na vitendo vyake vya unyanyasaji wa ngono ni msanii alieaga dunia Aaliyah maarufu kwa wimbo ‘Age ain’t nothing but a number”

Aaliyah

Baada ya wiki sita za ushahidi, mahakama ilijadili kwa saa tisa kabla ya kumpata na hatia nyota huyo mwenye umri wa miaka 54, R.Kelly amepatikana na hatia ya kuwaajiri wanawake na watoto kwa ajili ya ngono, kabla ya kufanya nao mapenzi na kuwafanyia ukatili.

Uamuzi huo unakuja miaka 13 baada ya Kelly kufutiwa mashtaka ya ponografia ya watoto baada ya kushtakiwa katika jimbo la Illinois.

Madai mengi yaliyosikilizwa katika kesi hiyo yalionyeshwa kwenye filamu fupi ya mwaka 2019 ya “Surviving R Kelly”.

R.Kelly alifahamika kwa muziki mtondo wa R ‘n’B, na kwa miaka mingi alijijenga kama mwimbaji na mtayarishi wa muziki. Mzaliwa wa Chicago jimbo la Illinois,ameshinda tuzo 26 za Grammy na alitayarisha albamu ya msanii Aaliyah “Age Ain’t Nothing But A Number.”

Hukumu ya R.Kelly itafanyika Mei 4. Waendesha mashtaka wanasema Kelly huenda akahukumiwa kifungo kisichopungua miaka 10 gerezani au hata kifungo cha maisha.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted