Maafisa wa serikali Burundi walio na uhusiano wa kando kufutwa kazi

Rais Ndayishimiye anasema agizo hilo ni kwa heshima ya mwendazake rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aliyekuwa ameokoka

0
Evariste Ndayishimiye, Rais wa Burundi

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ameamua kuwafuta kazi wafanyakazi wote wa serikali walio na uhusiano wa kando. Rais Ndayishimiye alitangzaza haya kama hatua moja wapo yakuhakikisha kuwa Burundi inakuwa taifa lenye watu wenye maadili.

Kulingana na maagizo kama yalivyotolewa na Waziri wa Usalama wa Ndani Gervals Ndirakobuca , kila afisa wa serikali mwenye suria huenda akafutwa kazi.

Taarifa rasmi kutoka kwa Rais Ndayishimiye

“Kila afisa wa serikali atakayepatikana na hatia ya kutoka nje ya ndoa yake atafutwa kazi mara moja.Hii ni katika juhudi za kuhakikisha nchi inakuwa na maadili,” alisema Waziri Ndirakobuca.

Rais Evariste Ndayishimiye anasema agizo hilo ni kwa heshima ya mwendazake rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aliyekuwa ameokoka. Mnamo Mei 2017, kabla ya kifo chake, Rais Nkurunziza alikuwa ametangaza azimio lake la kutaka jamii izingatie maadili.

Rais Nkurunziza alikuwa amepitisha sheria kuwa wapenzi wote nchini humo wafunge ndoa halali ifikiapo Desemba 2017 au wachukuliwe hatua za kisheria. Kulingana na Nkurinziza kulikuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu lililosababishwa na wanaume waliopachika wasichana wengi ujauzito kwa wakati mmoja.

Maagizo yake Rais Ndayishimiye yamezua hali ya wasiwasi nchi Burundi na hali ya taharuki kati ya maafisa wa serikali.

Rais Ndayishimiye, aliapishwa Juni 18 2020, baada ya kuaga dunia kwa mtangulizi wake Rais Nkurunziza.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted