Bilionea Jeff Bezos kujenga hoteli ya kitalii katika anga za mbali

Kituo hicho kitakuwa na ukubwa wa futi 32,000 mraba kitawapa wateja fursa ya kuzalisha filamu,kufanya utafiti na nafasi ya hoteli ya kitalii

0
Mfano wa kituo hicho cha Orbital Reef

Kampuni ya utalii ya anga za mbali Blue Origin inayomilikiwa na mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, imetangaza mipango ya kuzindua kituo cha utalii katika anga za mbali. Hoteli hiyo ya anga za mbali  “Orbital Reef” inatarajiwa kuanza kukaribisha wageni mwishoni wa muongo huu,watalii 10 pekee wataruhusiwa kukaa kwa hoteli hiyo kwa wakati mmoja.

Mfano wa chumba kwenye hoteli ya Orbital Reef

Blue Origin itashirikiana na Sierra Space na Boeing kujenga kituo hicho, ikisema kuwa kituo hicho kitakuwa na ukubwa wa futi 32,000 mraba kitawapa wateja fursa ya kuzalisha filamu,kufanya utafiti nafasi ya hoteli ya kitalii ya anga za mbali.

Katika hotuba kwa wanahabari, maafisa wakuu watendaji kutoka Blue Origin na SIerra Space hawakuweka wazi kiasi cha pesa kitakachotumika kujenga kituo hicho, ila mradi huo utafadhiliwa kwa kiasi kikubwa na Jeff Bezos ambaye amejitolea kutoa $1 bilioni kila mwaka kwa mradi huo wa Blue Origin.

Jeff Bezos, mmiliki wa Amazon na Blue Origin
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted