Facebook yabadili jina na kuwa Meta

Mark Zuckerberg, aliyeanzisha Facebook mwaka wa 2004, alitangaza Alhamis jina jipya la Facebook

0
JIna jipya na nembo ya Facebook

Faceboook yabadili jina na kuwa Meta, Afisa mkuu mtendaji Facebook Mark Zuckerberg alitangaza hayo Alhamis.

Mark Zuckerberg na Facebook wamekuwa wakichunguzwa na wabunge na wadhibiti ndani na nje ya nchi, baada ya wafanyakazi wa zamani  kuweka wazi baadhi ya mienendo isiyofaa ya kampuni hiyo, mienendo ambayo imeipa sifa mbaya Facebook.

Mmoja wa wafanyakazi wa zamani France Haugen, ameishutumu kampuni hiyo kwa “kuzingatia zaidi kupata faida kuliko usalama wa wateja wake’.

Mark Zuckerberg, aliyeanzisha kampuni hiyo mwaka wa 2004, alitangaza Alhamis jina jipya la Facebook.

Mark Zuckerberg, Mwanzilishi wa Facebook

”Kampuni yetu sasa ni Meta”. amesema Zuckerberg, alipokuwa akizungumza katika mkutano uliofanywa kupitia mtandao, alisema kubadili jina kunaakisi matarajio ya kampuni kujenga “metaverse’ ambayo ndio muelekeo mpya baada ya mafanikio ya matumizi ya mtandao kwenye simu.

“Kupitia metaverse utaweza kufanya chochote kile utakachofikiria,utapatana na jamaa na marafiki,kufanya kazi,kujifunza, kucheza, kuuza na kununua na mambo mengine mengi ambayo kwa sasa huwezi kuyafanya kupitia tarakilishi au simu.” Mark Zuckerberg.

Ikiwa na watumiaji wapatao bilioni 2.9 kila mwezi, kampuni hiyo imekabiliwa na uchunguzi hususan baada ya mfanyakazi wa zamani, Frances Haugen kuvujisha nyaraka zilizoipa Facebook sifa mbaya, akijibu shtuma hizo Zuckerberg alisema nyaraka hizo zimetumiwa kumharibia sifa.

Kampuni hiyo  ilizindua nembo mpya katika makao makuu yake  eneo la Menlo Park, mjini California siku ya Alhamisi, ikibadilisha nembo yake ya thumbs-up “Like” na umbo la rangi ya bluu.

Nembo mpya ya Meta
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted