Kirusi kipya cha UVIKO 19 chagunduliwa Afrika Kusini

Kirusi hicho kwa jina la kisayansi B.1.1.529 kimegunduliwa pia nchini Botswana na Hong Kong miongoni mwa wasafiri kutoka Afrika Kusini.

0
Kirusi cha UVIKO 19

Wanasayansi nchini Afrika Kusini walisema Alhamisi wamegundua kirusi kipya cha UVIKO19. Madaktari wanalaumu kirusi hicho kwa ongezeko la idadi kubwa ya maambukizi.

“Habari mbaya ni kuwa tumegundua kirusi kipya ambacho kimesababisha wasiwasi nchini Afrika Kusini,” mtaalamu wa virusi Tulio de Oliveira aliambia wanahabari.

Kirusi hicho kwa jina la kisayansi B.1.1.529 kimegunduliwa pia nchini Botswana na Hong Kong miongoni mwa wasafiri kutoka Afrika Kusini.

Waziri wa Afya Joe Phaahla alisema kirusi hicho kimezua “wasiwasi mkubwa” na kimechangia ongezeko la visa vipya vya UVIKO 19.

Visa 1,200 viliripotiwa siku ya Jumatano, baada ya visa vya maambukizi kuongezeka kutoka visa 100 kwa siku hadi zaidi ya visa 1000 kwa siku mwezi Novemba.

Mwaka jana Afrika Kusini iligundua kirusi cha Beta ila maambukizi mapya yametokana na kirusi cha Delta ambacho kiligunduliwa mara ya kwanza nchini India.

Afrika Kusini ina idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya UVIKO 19 barani Afrika, ikiwa na kesi milioni 2.95 na takriban watu 89,657 wakifariki kutokana na ugonjwa huo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted