UN inakadiria kuwa mtu mmoja 1 kati ya 3 duniani kote hajawahi kutumia mtandao

Inakadiriwa kuwa 37% ya idadi ya watu wote duniani, karibu watu bilioni 2.9, hawajawahi kutumia mtandao

0

Inakadiriwa kuwa asilimia 37 ya idadi ya watu duniani, karibu watu bilioni 2.9, hawajawahi kutumia mtandao, hayo ni kulingana na data kutoka Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU), wakala ndani ya Umoja wa Mataifa.

Licha ya takwimu hii, ITU imeona ukuaji mkubwa katika matumizi ya mtandao kote ulimwenguni. Idadi ya wale ambao wamekuwa mtandaoni imeongezeka hadi bilioni 4.9 mnamo 2021, kutoka bilioni 4.1 mnamo 2019.

Ongezeko ya idadi ya watumiaji wa mtandao huenda ilichangiwa na janga la UVIKO -19 na kampeni zilizoendeshwa wakati wote wa janga hili wakati marufuku ya kutotoka nje iliwekwa na kuwalazimu watu kutumia mitandao kurahisisha maisha ya kila siku.

Hiyo ilileta takriban watumiaji milioni 782 zaidi wa mtandao, na kuongeza muunganisho wa mtandao kwa asilimia 17 kutoka 2019, ilisema ITU.

Kati ya watu ambao hawajaunganishwa kwenye Intaneti, asilimia 96 wanaishi katika mataifa yanayoendelea. Na ingawa watu bilioni 4.9 ni watumiaji wa mtandao, ITU ilisema kuwa mamilioni yao wana uwezekano wa kutumia intaneti mara chache zaidi kuliko wale walio katika nchi zilizoendelea na wanaweza kutumia intaneti kwa kasi isiyofaa ikilinganishwa na wale walio katika mataifa tajiri.

“Wakati karibu theluthi mbili ya watu duniani sasa wapo mtandaoni, kuna mengi zaidi ya kufanya ili kila mtu aunganishwe kwenye Mtandao,” Katibu Mkuu wa ITU Houlin Zhao alisema, kulingana na taarifa ya ITU kwa vyombo vya habari.

“ITU itashirikiana na pande zote kuhakikisha kwamba vitalu vya ujenzi vinawekwa ili kuunganisha watu bilioni 2.9 ambao hawafikii huduma za mtandano. Tumedhamiria kuhakikisha hakuna atakayeachwa.”

Mtandao umekuwa zana muhimu kwa Wamarekani wakati wa janga la UVIKO -19, haswa mapema mwaka wa 2020.

Kura ya maoni ya Kituo cha Utafiti cha Pew iliyotolewa mnamo Septemba ilionyesha kuwa asilimia 90 ya Wamarekani walisema mtandao umekuwa muhimu kwao wakati wa janga la UVIKO 19.

Asilimia themanini na moja ya Wamarekani pia walisema walikuwa wamezungumza na wengine kupitia simu za video tangu janga hilo lilipoanza mnamo Februari 2020, kulingana na Pew.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted