Waziri Mkuu wa zamani ashtakiwa kwa mauaji ya mke wake

Waziri Mkuu wa zamani wa Lesotho Thomas Thabane ameshtakiwa kwa mauaji ya mke wake

0
Thomas Thabane, waziri mkuu wa zamani wa Lesotho

Waziri Mkuu wa zamani wa Lesotho Thomas Thabane ameshtakiwa kwa mauaji ya mke wake Lipolelo Thabane ya mwaka 2017. Mke wake wa sasa, Maesaiah, alishtakiwa kwa uhalifu huo mwaka jana.

Maesaiah alikuwa akiishi na Bw Thabane wakati wa mauaji hayo na wanashutumiwa kwa kuajiri wauaji waliotekeleza uhalifu huo. Wote wawili wamekana kuhusika.

Bw Thabane alijiuzulu mwezi Mei 2020 kufuatia shinikizo la miezi kadhaa baada ya kutajwa kama mshukiwa.

Kesi hiyo imeshangaza wengi na kusababisha misukosuko ya kisiasa katika nchi hiyo ndogo ya kifalme.

Maesaiah Thabane aliandamana na waziri mkuu huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 82 hadi mahakamani. Maesaiah alishtakiwa mwaka jana na kisha kuachiliwa kwa dhamana.

Mashtaka hayo yalisomwa katika ukumbi wa Mahakama Kuu katika mji mkuu wa Maseru, badala ya katika chumba cha mahakama kuu, jambo ambalo ni la kawaida, shirika la habari la AFP linaripoti.

Watu wenye silaha walimpiga risasi na kumuua Lipolelo Thabane tarehe 14 Juni 2017 – siku mbili kabla ya Bw Thabane kuapishwa kama waziri mkuu.

Lipolelo alivamiwa na kupigwa risasi mara kadhaa barabarani alipokuwa akirudi nyumbani, alifariki kando ya barabara. Alikuwa na umri wa miaka 58.

Wakati huo, Lipolelo alikuwa kwenye mchakato wa kutalakiana na Bw Thabane na alikuwa akiishi kando na mumewe tangu 2012. Thabane nae alikuwa akiishi na Maesaiah kati ya 2012 na 2017. Walioana miezi miwili baada ya kifo cha Lipolelo.

Maesaiah Thabane na Thomas Thabane

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted