Nigeria: Msongamano na mashambulizi katika magereza

Nigeria inashikilia nafasi ya 49 katika orodha ya nchi 206 zenye msongamano mkubwa wa wafungwa kwenye magereza yao

0

Mwezi uliopita, watu wenye silaha walivamia gereza lenye ulinzi wa kati huko Jos, katikati mwa Nigeria, kwa mara ya pili mwaka huu, na kufanikiwa kuwaachia huru zaidi ya wafungwa 250.

Lilikuwa ni tukio la hivi punde zaidi katika msururu wa kuvamiwa kwa jela ambayo imekuwa ikitokea katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika tangu 2010.

Zaidi ya watu 7,000 wametoroka kutoka magereza kadhaa katika kipindi hicho, huku wengi wao hawajulikani walipo. Katika kipindi cha miezi 14 pekee, kumekuwa na visa nane vya wafungwa kutoroka jela ikiwa ni mara mbili zaidi kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Idadi ya waliotoroka haijumuishi ghasia, majaribio ya kutoroka au mapigano kati ya wafungwa na walinda usalama kwenye gereza hizo.

Mwezi uliopita, maafisa wa usalama walizuia jaribio la wahalifu waliotaka kumteka nyara mshukiwa kutoka jengo la mahakama ya Lagos ambako alikuwa akisikiliza kesi dhidi yake.

Mfumo wa magereza wa Nigeria kwa muda mrefu umekumbwa na matatizo mengi. Kanuni za jinai na adhabu za nchi hiyo ni za zamani, wakati miundo msingi ni masalio ya enzi ya ukoloni wa Uingereza. Magereza mengi hayawezi kuhimili idadi kubwa ya wafungwa kwenye magereza ya sasa.

Kuchangia zaidi ni kuwa magereza hayo ni baadhi ya magereza yenye msongamano mkubwa zaidi duniani.  Nigeria inashikilia nafasi ya 49 katika orodha ya nchi 206 zenye msongamano mkubwa kwenye magereza yao, orodha iliyochapishwa na Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Uhalifu na Haki ya Chuo Kikuu cha London.

Kwa mfano, Gereza la Ikoyi, lililojengwa mwaka wa 1955 ili kushikilia wafungwa 800, sasa linashikilia wafungwa takriban mara nne ya idadi hiyo.

Kulingana na NCS, kwa sasa kuna wafungwa 70,653 katika magereza 240 kote nchini. Ni theluthi moja tu kati yao wametiwa hatiani huku wengine wakisubiri kusikiliza kesi zao.

Wafungwa wengi ni washukiwa ambao wamefungwa kwa miaka mingi kwa makosa madogo kama vile wizi madukani na makosa ya trafiki. Katika baadhi ya magereza wale wanaosubiri kusikilizwa kwa kesi zao wanawakilisha hadi asilimia 90 ya jumla ya wafungwa, ambao idadi yao halisi inaaminika kuwa kubwa zaidi kuliko ile ya wafungwa ambao walipatikana na hatia.

Kwa hivyo, magereza yamekuwa maeneo rahisi kwa kila aina ya mashambulizi katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa makundi yenye silaha au watu wenye silaha wasiojulikana, na ghasia za wafungwa.

Vituo vya kurekebisha tabia huko Kogi pia vimeshambuliwa na wafungwa na Boko Haram mara mbili.Mashambulizi mara nyingi husababisha majeruhi wengi. Katika tukio la hivi punde zaidi katika gereza la Jos, takriban watu 10 waliuawa na saba kujeruhiwa vibaya.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted