Wachimba migodi 31 wauawa baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka

Takriban wachimbaji wadogo milioni mbili huzalisha takriban 80% ya dhahabu kila mwaka ikiwa ni takriban tani 80, kulingana na takwimu rasmi.

0

Takriban wachimba migodi 31 wameuawa na wanane kutoweka nchini Sudan Jumanne wakati mgodi wa dhahabu ulipoporomoka, afisa wa serikali amesema.

Maafa hayo yametokea karibu na Nuhud, mji ulio umbali wa kilomita 500 (maili 310) magharibi mwa Khartoum, alisema Khaled Dahwa, mkuu wa Kampuni ya Rasilimali za Madini inayomilikiwa na serikali huko Kordofan Magharibi.

“Wachimbaji madini wa jadi 31 wameua baada ya mgodi kuporomoka,”aliiambia AFP, na kuongeza kuwa mtu mmoja alinusurika na wengine wanane bado hawajulikani walipo.

Uchimbaji madini ya dhahabu ni taaluma hatari nchini Sudan kwa kiasi kikubwa kutokana na miundombinu mibovu.

Uchimbaji migodi ulistawi takriban muongo mmoja uliopita katika sehemu mbalimbali za nchi, huku watu wakichimba ardhi kwa kutumia mashini zisizostahili kwa matumaini ya kuchimbua madini hayo ya thamani.

Takriban wachimbaji wadogo milioni mbili huzalisha takriban asilimia 80 ya dhahabu kila mwaka ikiwa ni takriban tani 80, kulingana na takwimu rasmi.

Sudan ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, hivi karibuni imekumbwa na mfumko wa bei na kuanza mageuzi magumu ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupunguza ruzuku ya petroli na dizeli.

Pia inakumbwa na msukosuko wa kisiasa kufuatia mapinduzi yaliyoongozwa na mkuu wa kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan mnamo Oktoba 25.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted