Polisi watumia mabomu kuwatawanya Wamachinga

Ni baada ya wafanyabiashara hao kuishinikiza Serikali iwaache waendelee kufanya biashara

0

Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam, limejikuta likitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wadogo wa soko la karume walioandamana hadi ofisi ya mkuu wa mkoa huo.

Tukio hilo limetokea leo baada ya wafanyabiashara hao kukaidi maagizo ya Serikali, yaliyowataka kuwa wavumilivu wakati ambapo uchunguzi unafanyika kujua chanzo cha kuwaka moto katika soko hilo ambalo wamekuwa wakifanya biashara zao

Mapema leo asubuhi wafanyabiashara hao waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam bwana Amosi Makala wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea na biashara katika soko hilo lililoungua usiku wa kuamkia Januari 16,2022.

Wafanyabiashara hao maarufu kama machinga mbali na kufanya maandamano pia wamefunga barabara kwa kuweka magogo na mawe katikati ya barabara ya makutano ya Uhuru na Kawawa eneo la Ilala Boma.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted