CCM kuchuja waliowania kuchukua kiti cha Uspika

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho leo itakaa kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea hao

0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Rais Samia Suluhu Hassan

Kikao  cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinafanyika leo katika ofisi za Makao Makuu (White House) jijini Dodoma.

Kikao hicho kimetanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika jana, kwa ajili ya kujadili wagombea 71 na kuishauri Kamati Kuu wagombea waliojitokeza kuomba kiti hicho cha uspika.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka alisema jana: “Januari 19, 2022 kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekutana kwa ajili ya kujadili wagombea waliojitokeza kuomba nafasi ya uspika na kuishauri Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.” Kwa mujibu wa ratiba ya awali, Kamati Kuu itafanya kazi ya kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho.

Kikao hicho kitafuatiwa na kikao cha chama cha wabunge wa CCM ambacho kitapiga kura kumpata mgombea ambaye atakwenda kusimama bungeni kwa ajili ya kuomba kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge.

Jumla ya wana CCM 71 walijitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo wakiwemo wanaume 60 na wanawake 11. Kati ya waliochukua fomu, wawili kati yao walishindwa kurudisha fomu hizo.

Waliojitokeza kuchukua fomu ni Samweli Mageto, Rahimuddin Ismail, Alex Msama, Themistocles Rwegasira, Dk Thomas Kashililah, Luhaga Mpina, Hatibu Madata, Dk Linda Ole Saitabau, Profesa Norman Sigalla King, Emmanuel Sendama, Goodluck Milinga, Bibie Msumi, Hilal Seif na Athumani Mfutakamba.

Wengine ni Mwenda Burton Mwenda, Herry Kessy, Josephat Malima, Adam Mnyavanu, Stella Manyanya, Andrew Kevela, Hussein Mataka, Hatibu Mgeja, Ezekiel Maige, Emmanuel Mng’arwe, Aziz Mussa, Onyango Otieno, Doto Mgasa, Profesa Edison Lubua, Fikiri Said, Profesa Itikija Mwanga na Peter Njemu.

Wamo pia Ndurumah Mejembe, Godwin Maimu, Johnson Japhet, Mohamed Mmanga, Esther Makazi, Mariam Moja, Joseph Anania, Samweli Xaday, Arnold Peter, Joseph Sabuka, Andrew Chenge, Dk Titus Kamani, Dk Mussa Ngonyani, Faraji Rushagama, Hamisi Rajabu na Asia Abdallah.

Festo Kipate, George Nangale, Barua Mwakilanga, Zahoro Haruna, Thomas Kirumbuyo, Angelina John, Abdilaziz Jaaf Hussein, Mussa Zungu, Emmanuel Mwakasaka, Profesa Hadley Mafwenga, Joseph Msukuma, Goodluck Ole Medeye, Sophia Simba, Juma Hamza Chum, Baraka Byabyato, Simon Ngatunga, Tumsifu Mwasamale, Merkion Ndofi, Dk Tulia Ackson, Godwin Kunambi, Ambwene Kajula, Patrick Nkandi, Steven Masele na Hamidu Chamami.

Spika atakayepatikana atakuwa wa saba tangu Uhuru – akiwa ametanguliwa na Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Erasto Mang’enya, Pius Msekwa, Samuel Sitta, Anne Makinda na Job Ndugai aliyejiuzulu wadhifa huo mapema mwezi huu kutokana na shinikizo baada ya kutoa kauli iliyogonganisha mihimili ya Bunge na Serikali.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted