Watu wanne na mtoto waganda kwa baridi hadi kufa katika mpaka wa US-Canada

Nyuzi joto siku ambapo miili hiyo ilipopatikana, ilikuwa nyuzi 35 chini ya Selsiasi.

0
Mpaka wa Amerika na Canada

Mamlaka ya Canada ilipata miili ya watu wanne akiwemo mtoto mchanga ambaye inaonekana aliganda hadi kufa katika tufani ya theluji mita chache kutoka mpaka wa Amerika kwenye njia inayotumiwa na wahamiaji, maafisa walisema Alhamisi.

Nyuzi joto siku ya Jumatano wakati miili hiyo ilipopatikana katikati ya maporomoko makubwa ya theluji, ikizingatiwa upepo, ilikuwa nyuzi 35 chini ya Selsiasi.

“Katika hatua hii ya kwanza ya uchunguzi, inaonekana kwamba wote walikufa kwa sababu ya baridi nyingi,”  Polisi wa Canada walisema katika taarifa.

Miili ya watu wazima wawili na mtoto mchanga ilipatikana takriban mita 12  kutoka mpaka na Amerika takriban kilomita 10 kutoka mji wa Emerson katikati mwa mkoa wa Manitoba.

Mwili wa mtu wa nne aliyeonekana kuwa mvulana ulipatikana baadaye, polisi walisema.

Mapema siku hiyo, maajenti wa mpakani kwa upande wa Amerika waliwazuilia kundi la watu ambao walikuwa wamevuka mpaka na walikuwa na bidhaa za watoto lakini hawakuwa na mtoto.

Hii ilisababisha msako kuanza katika pande zote za mpaka.

Miili ya kwanza ilipatikana baada ya saa nne za upekuzi.

Wizara ya Sheria ya Amerika ilisema Alhamisi kuwa walimkamata mwanamume mmoja katika njia hiyo hiyo, wakimshtaki kwa ulanguzi wa binadamu.

Mzaliwa wa Florida mwenye umri wa miaka 47 alipatikana akiendesha gari na raia wawili wa India wasio na vibali  kusini mwa mpaka wa Canada, Idara ilisema, karibu na mahali ambapo kundi la wahamiaji lilikamatwa.

Uraia wa walioaga dunia haukutolewa, ingawa Idara ya Sheria ya Amerika ilisema “walitambuliwa kuwa kati ya kundi la watu wengine wahamiaji waliokamatwa awali.

Kamishna Msaidizi wa Manitoba Jane MacLatchy aliuambia mkutano wa awali wa waandishi wa habari kwamba aliwaona watu hawa kama waathiriwa.

Emerson ni njia ambayo wahamiaji hutumia kusafiri kati ya Amerika na Canada.

Majaribio ya kuvuka yamepungua kwa muda wa mwaka sasa kwa sababu mpaka umefungwa kutokana na janga la UVIKO 19 alisema MacLatchy.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted