Watu watano watekwa nyara kutoka shuleni Cameroon

Watu wanaotaka kujitenga mara kwa mara hushambulia shule ambazo wanazituhumu kufundisha kwa Kifaransa, na kuua watumishi wa umma.

0

Walimu watatu, mwalimu mkuu na naibu wake walitekwa nyara kutoka shule ya upili ya Cameroon na watu wenye silaha. Utekajinyara huo ulitekelzwa katika moja ya mikoa miwili inayozungumza Kiingereza iliyokumbwa na vita kati ya watu wanaotaka kujitenga, chama cha walimu kiliiambia AFP siku ya Ijumaa.

“Kundi lililojihami lilivamia shule ya upili ya Weh siku ya Jumanne na kuwateka nyara watu watano,” alisema Roger Kafo, katibu mkuu wa Muungano wa Kitaifa wa Walimu wa Sekondari (Snaes).

Watu wanaotaka kujitenga mara kwa mara hushambulia shule ambazo wanazituhumu kufundisha kwa Kifaransa, na kuua watumishi wa umma, wakiwemo walimu, ambao wanawatuhumu “kushirikiana” na serikali kuu ya Yaounde.

Wanafunzi wametekwa nyara na baadaye kuachiliwa.

“Kwa sasa hatuna habari zozote kuhusu mateka na hakuna aliyeachiliwa,” Kafo aliongeza.

Waliotekwa ni mwalimu mkuu, naibu wake na walimu watatu.

Maeneo ya kaskazini-magharibi na kusini-magharibi yamekumbwa na ghasia tangu mwaka wa 2017 wakati wapiganaji wanaozungumza lugha ya Kiingereza walipotangaza uhuru kutoka kwa nchi hiyo yenye watu wengi wanaozungumza Kifaransa.

Yaounde alijibu kwa kuzima makundi hayo.

Wanajeshi wanaotaka kujitenga na vikosi vya serikali wameshutumiwa kwa ukatili katika mapigano hayo, ambayo yamegharimu maisha ya zaidi ya watu 3,000 na kuwalazimu zaidi ya 700,000 kukimbia makazi yao.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted