Kenya: Waziri wa Elimu Prof.Magoha azungumzia mkanganyiko ulioko kuhusu mfumo mpya wa CBC

Profesa Magoha alisisitiza kuwa wanafunzi wa kwanza wa mfumo wa CBC hawatarejea katika mfumo wa zamani wa 8-4-4.

0
Waziri wa Elimu Prof George Magoha

Waziri wa Elimu Prof George Magoha amezungumzia wasiwasi ulioko kati ya wazazi kuhusu masomo ya wanafunzi wa darasa la sita kujiunga na shule za upili.

Akihutubia wanahabari Ijumaa, Februari 11, katika Kaunti ya Siaya, Waziri alisema kuwa shule za upili katika mtaala mpya wa CBC  zitakuwa katika shule za upili.

Alisisitiza kuwa wanafunzi wa kwanza wa mfumo wa CBC hawatarejea katika mfumo wa zamani wa 8-4-4.

Wanafuzi wa darasa la sita katika mfumo mpya wa CBC wanatarajiwa kufanya mtihani wao wa kitaifa mwezi Desemba.

“Wanafunzi hao watajiunga na shule za sekondari baada ya mtihani huo, tunalenga kujenga madarasa 20,000.

“Mchakato wa wanafunzi kujiunga na darasa la Saba yatafanyika bila mimi kuwepo lakini maagizo ya Rais Uhuru Kenyatta ni kwamba tujiandae na kuacha kila kitu kikiwa sawa.”

“Kwa mfano, mtihani wa darasa la sita mwezi Desemba uko tayari,” CS alisema. Magoha alizidi kuwakashifu wadau mbalimbali wa elimu ambao wanataka kurejeshwa kwa mfumo wa 8-4-4 kwa waanzilishi wa darasa la CBC.
“Sidhani kama kuna mtu ataweza kuzuia hili kwa sababu baada ya miezi miwili tutakuwa na waanzilishi wa CBC wa Daraja la Sita na itakuwa ni wendawazimu kufikiria kuwa wanafunzi hawa watarejeshwa kwenye mfumo wa zamani.”

Aliongeza kuwa ujenzi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya shule za upili unaofanywa nchini umepiga hatua, akiongeza kuwa Ksh3.2 bilioni zimetengwa kwa mradi huo.

Hata hivyo, alifichua kuwa kazi za ujenzi katika shule hizo zitachukua mapumziko wakati wa mtihani wa shule za sekondari wa (KCSE) ambao umeratibiwa kuanza mwezi Machi.

Zaidi ya hayo, alisema kuwa walimu ambao walipata mafunzo kuhusu mtaala mpya wa CBC ndio watakaofunza katika shule za upili za CBC.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted