Uganda: Uzinzi Sio Uhalifu, Polisi wasema

Mnamo 2007, Mahakama ya Kikatiba iliamua kwamba uzinzi haikuwa tena kosa la jinai nchini Uganda baada ya kuifuta kutoka kwa Kanuni ya Adhabu.

0

Polisi nchini Uganda wamesema kuwa uzinzi sio uhalifu na kwa hivyo hauwezi kuripotiwa kwa polisi kwa lengo la kukamatwa kwa mtu.

Wiki iliyopita kulikuwa na tukio ambapo mtangazaji wa TV alirekodiwa kwenye kamera na kunaswa akiwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke aliyeolewa.

Maafisa wa polisi waliohusika katika kesi hiyo wametiwa mbaroni kwa kuhusika na kesi hiyo ambayo si uhalifu, iwapo polisi hao watapatikana na hatia wanaweza kutimuliwa kwao kutoka kwa jeshi.

Akihutubia wanahabari Jumatatu, msemaji wa Polisi, Fred Enanga alisema uzinzi si kosa ila ni suala la kiraia.

“Uzinzi si kosa tena katika nchi yetu, hivyo kuufanya kuwa uhalifu ni kitendo kisicho cha kitaalamu na iwapo mtu atakamatwa na polisi kwasababu ya hilo basi itakuwa matumizi mabaya ya mamlaka jambo ambalo polisi haliwezi kuvumilia,” alisema Enanga.

Msemaji huyo wa polisi aliwaonya watu waliooko katika mifumo yoyote ya ndoa kuheshimu utakatifu wa ndoa na kutumia njia halali, badala ya kuchafua sifa za wapenzi wao.

Alibainisha kuwa ingawa uzinzi sio uhalifu, hata hivyo, unaweza kutumika kama msingi wa michakato kama vile kudai talaka, kutengana, malezi ya watoto na kugawana mali iwapo mmoja katika ndoa alipatikana katika uzinzi

Mnamo 2007, Mahakama ya Kikatiba iliamua kwamba uzinzi haikuwa tena kosa la jinai nchini Uganda baada ya kuifuta kutoka kwa Kanuni ya Adhabu.

Hapo awali, ingawa sheria ya uzinzi ilitaja adhabu na masuluhisho tofauti kwa wanaume na wanawake, ilidhaniwa hapo awali kwamba wanaume walioko katika ndoa tu ndio wangeweza kuathrika kutokana na kesi ya uzinzi.

Kama adhabu, mume aliyedhulumiwa angelipwa fidia ya Ush600 ambayo baadaye ilipanda hadi Ush1,200, lakini mke aliyedhulumiwa hakupata chochote.

Hata hivyo, katika uamuzi wa kihistoria kufuatia ombi la wanaharakati wanawake chini ya Sheria na Utetezi wa Wanawake, mahakama hiyo kwa kauli moja ilikubali kuwa kifungu cha 154 cha sheria ya kanuni ya adhabu inayoharamisha uzinzi ni kinyume cha katiba kwa sababu ilitoa adhabu tofauti kwa wanaume na wanawake na hivyo kukitupilia mbali kutoka kwa Kanuni ya Adhabu.

.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted