Idadi ya vifo kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi Brazil imeongezeka hadi 104

Mji wa Petropolis Brazil Wafanyakazi wa uokoaji wamefanya kazi usiku na mchana kutafuta manusura wowote waliosalia kati ya matope na mabaki baada ya mafuriko makubwa na maporomoko ya...

0
Mji wa Petropolis Brazil

Wafanyakazi wa uokoaji wamefanya kazi usiku na mchana kutafuta manusura wowote waliosalia kati ya matope na mabaki baada ya mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi kupiga jiji la Petropolis nchini Brazili, huku mamlaka ikisema Alhamisi kwamba idadi ya waliofariki imeongezeka hadi 104.

Mitaa iligeuzwa kuwa kama mito yenye mafuriko na nyumba zilisombwa baada ya dhoruba kali kuleta mvua kubwa katika muda wa saa tatu kwenye mji wa kitalii uliopo karibu na Rio de Janeiro.

Huku watu kadhaa wakiripotiwa kutoweka, hofu kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka imepelekea wazima moto na watu wa kujitolea kuwatafuta manusura katika mabaki ya nyumba zilizosombwa na tope nyingi.

Ni dhoruba za hivi punde zaidi katika mfululizo wa dhoruba mbaya kuikumba Brazili katika muda wa miezi mitatu iliyopita, ambayo wataalam wanasema imekuwa mbaya zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Serikali ya jimbo hilo ilisema takriban watu 24 wameokolewa.

Wakitumia mbwa, wachimbaji na wafanyikazi wa uokoaji walikuwa wakitafuta manusura kabla muda mwingi kupita, huku ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma wa Rio ikiripoti kuwa watu 35 waliotoweka walikuwa wamesajiliwa.

Takriban watu 300 walikuwa waliwekwa kwa makazi mbadala, wengi wakiwekwa shuleni, maafisa walisema.

Mashirika ya misaada iliagiza kusaidiwa na michango ya magodoro, chakula, maji, nguo na barakoa kwa waathiriwa.

Video zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zilizonyesha mitaa ya Petropolis, ikiwa imejaa mafuriko ambayo yalisomba magari, miti na karibu kila kitu kingine katika mkondo wake.

Maduka mengi yalifunikwa kabisa na maji yaliyokuwa yakipanda, ambayo yalitiririka chini ya mitaa ya katikati mwa jiji la kihistoria, na kuacha mirundiko ya magari.

Maafisa walisema zaidi ya wazima moto 180 na waokoaji wengine walikuwa wakijibu dharura hiyo, wakisaidiwa na wanajeshi 400 waliotumwa kusaidia katika juhudi za uokoaji.

Afisi ya meya wa jiji ilisema mji huo wa watu 300,000 umekumbwa na maafa makubwa. Baraza la jiji lilitangaza siku tatu za maombolezo kwa wahasiriwa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted