Waziri wa zamani wa Morocco ahukumiwa kifungo baada ya video yake ya ‘uzinzi’ kusambaa mitandaoni

video inadaiwa kumuonyesha Zaine akiwa katika hali tata na mwanamke aliyeolewa kwenye chumba cha hoteli.

0

Waziri wa zamani wa haki nchini Morocco ambaye alikua mkosoaji mkubwa wa serikali alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela siku ya Jumatano kwa msururu wa mashtaka, wakili wake alisema.

Mohamed Ziane, 79, alikuwa amefikishwa mahakamani mwaka jana baada ya kushutumu idara za usalama za ufalme huo kwa kughushi video iliyodaiwa kumuonyesha akiwa katika hali tata na mwanamke aliyeolewa kwenye chumba cha hoteli.

Video hiyo ilizua kashfa, lakini Ziane alimshutumu mkuu wa polisi na vikosi vya usalama vya ndani vya Morocco, Abdelatif Hammouchi, kwa kughushi kanda hiyo.

Wizara ya mambo ya ndani mnamo Januari mwaka jana iliwasilisha malalamishi ikimtuhumu kwa jinai ya ‘kusambaza mashtaka ya uwongo.’

Mahakama ya Rabat siku ya Jumatano ‘ilimhukumu Bw Ziane kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya dirham 5,000 (kama dola 530),’ wakili Amal Khalfi alisema.

Lakini aliongeza kuwa ‘bado hatujui undani wa hukumu hiyo. Hatujui ni mashtaka gani yalizingatiwa.’

Ziane bado yuko huru akisubiri rufaa, alisema.

Waziri huyo wa zamani aliliambia shirika la habari la AFP mwezi Disemba kwamba alikabiliwa na jumla ya mashtaka 11, yakiwemo ‘dharau kwa maafisa wa umma na mahakama’ kukashifu, uzinzi na unyanyasaji wa kijinsia.

Alisema mashtaka dhidi yake ni ya kisiasa.

Ziane alikuwa mwanasheria mashuhuri wa serikali mwanzoni mwa miaka ya 1990 na waziri wa haki za binadamu kati ya 1995 na 1996. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, amekuwa mkosoaji maarufu wa mamlaka, hasa idara za usalama.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted