Google yasitisha kuonyesha matangazo kwa vyombo vya habari vya serikali ya Urusi

Kampuni ya Google imesema haitaruhusu tena vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kuonyesha matangazo, kufuatia uamuzi kama huo uliofanywa Jumamosi na kampuni mwenza ya video ya YouTube.

0

Kampuni ya Google imesema haitaruhusu tena vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kuonyesha matangazo, kufuatia uamuzi kama huo uliofanywa Jumamosi na kampuni mwenza ya video ya YouTube.

Google imesema ili kukabiliana na vita nchini Ukraine wanasitisha upatikanaji wa mapato wa Google kwa vyombo vya habari vinavyofadhiliwa na serikali ya Urusi kwenye mifumo yao yote na wanafuatilia kwa makini matukio mapya na watachukuwa hatua zaidi ikihitajika.

Tangazo hilo linakuja baada ya tangazo la hivi karibuni kwa vyombo vya habari vinavyohusishwa na Urusi huku kukiwa na wimbi la ukosoaji ulioelekezwa kwa majukwaa ya Big Tech katika wiki iliyopita kwa kuruhusu upataji wa mapato kuendelea licha ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Siku ya Ijumaa mtandao wa Meta (Facebook) ulisema utasitisha uwezo wa vyombo vya habari vya serikali vya Urusi kuendesha matangazo na kujipatia mapato kwenye majukwaa yake.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted