Mganga ambaka mwanafunzi kwa madai kuwa ni masharti ya dawa

Jeshi la Polisi Mkoani Lindi linamtafuta Juma Salumu maarufu ‘Juma kipanya’ ambaye ni mganga wa kienyeji mkazi wa Manispaa ya Lindi,anayedaiwa kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa...

0

Jeshi la Polisi Mkoani Lindi linamtafuta Juma Salumu maarufu ‘Juma kipanya’ ambaye ni mganga wa kienyeji mkazi wa Manispaa ya Lindi,anayedaiwa kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 15 Wilayani Lindi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Foka Dinya ameeleza kuwa Mama Mzazi wa Mtoto huyo aligundua Mtoto wake kuwa mjamzito mwezi Disemba 2021 na alitoa taarifa Polisi Februari 3, 2022 ambapo tayari Mganga huyo alikuwa ametorokea kusipojulikana.

Mama Mzazi wa Mtoto huyo amesema mwezi wa sita mwaka jana Mtoto wake alipelekwa kwa Mganga huyo na Babu yake kwa madai ya kwenda kutengeneza dawa baada ya Mganga kutoa sharti la dawa yake ni lazima itengenezwe na Binti kigoli yaani binti asiyewahi kushiriki tendo la ndoa wala kuzaa, na alipopelekwa Binti huyo mganga alimbaka kisha kumtishia asiseme kwa Watu kwani akisema mizimu itampa adhabu.

Mama huyo amesema Binti yake aliporudi nyumbani hakusema chochote na aliendelea na masomo yake mpaka ilipofika December 2021 ambapo waligundua hali isiyokuwa ya kawaida na walipombana akaeleza kwamba alibakwa na mganga Juma Salum alipokwenda kutengeneza dawa ya Babu yake.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted