Mwendesha mashtaka: ICC kuanza uchunguzi kuhusu hali ‘ilivyo nchini Ukraine’

“Nimeridhika kwamba kuna msingi mzuri wa kuamini kwamba uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu umefanywa nchini Ukraine” tangu 2014, Karim khan

0
Mahakama ya ICC The Hague Uholanzi

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC Karim Khan alisema Jumatatu alikuwa akianzisha uchunguzi kuhusu ‘hali nchini Ukraine’ kufuatia uvamizi wa Urusi.

“Leo ningependa kutangaza kwamba nimeamua kuanza uchunguzi kuhusu hali ya Ukraine, haraka iwezekanavyo,” Khan alisema katika taarifa yake.

“Nimeridhika kwamba kuna msingi mzuri wa kuamini kwamba uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu umefanywa nchini Ukraine” tangu 2014, aliongeza.

“Kwa kuzingatia kuongezeka kwa mzozo katika siku za hivi karibuni, ni nia yangu kwamba uchunguzi huu pia utajumuisha uhalifu wowote mpya unaodaiwa kuwa chini ya mamlaka ya ofisi yangu ambao unafanywa na upande wowote kwenye mzozo katika sehemu yoyote ya eneo la Ukraine.”

Khan alisema wiki jana kwamba mahakama hiyo yenye makao yake The Hague ilipokea maswali mengi “kuhusiana na uhalifu na uchokozi” lakini haikuweza kutumia ‘mamlaka yake  juu ya uhalifu huu unaodaiwa’ kwani Urusi na Ukraine hazijatia saini Mkataba wa Roma ulioanzisha na ICC.

“Nitaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo nchini Ukraine, na tena nitoe wito kwa kuzingatiwa kwa sheria za kimataifa za kibinadamu,” alisema Jumatatu.

Mwaka wa 2014 na 2015 Ukraine ilitambua uwezo wa ICC kuchunguza madai ya uhalifu wakati na baada ya kuanguka kwa kiongozi anayeunga mkono Urusi Viktor Yanukovych na baada ya uvamizi wa Urusi huko Crimea, aliongeza.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted