Wahamiaji tisa wazama karibu na Tunisia

Shirika la UN la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema takriban wahamiaji 1,300 walitoweka au kufa maji mwaka jana katika bahari ya Mediterania.

0

Wahamiaji tisa walikufa maji siku ya Jumatatu baada ya mashua yao kupinduka katika pwani ya Tunisia wakati wa harakati za kufika Ulaya, wizara ya ulinzi ilisema.

Miili ya wahamiaji hao, ‘raia wa nchi mbalimbali za Afrika’ iliopolewa na askari wa majini na walinzi wa pwani katika mkoa wa Al-Mahdia kwenye pwani ya Mediterania.

Abiria wengine tisa waliokolewa, wizara ilisema katika taarifa yake.

Ikinukuu manusura,mamlaka ilisema mashua hiyo iliondoka Jumapili usiku kutoka mji wa bandari wa Sfax ‘kwa nia ya kuvuka kinyume cha sheria’ kuelekea Ulaya.

Italia ni kimbilio kuu la wahamiaji wanaokimbilia eneo la Uropa kwa boti kutoka Tunisia na Libya, katika kile ambacho mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema ndiyo njia mbaya zaidi ya uhamiaji duniani.

Uhamiajai umeongezeka tangu maasi katika nchi zote mbili yawaondoe viongozi wao mwaka 2011.

Wakati wengi wa wahamiaji hao wanatoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, watu wa Tunisia wameongezeka pia katika safari hizi hatari za kutafuta maisha bora.

Kundi la haki za FTDES la nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika linasema kuwa katika miezi tisa ya kwanza ya 2021, walinzi wa pwani waliwakamata wahamiaji 19,500 wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema takriban wahamiaji 1,300 walitoweka au kufa maji mwaka jana katika bahari ya Mediterania.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted