Amuua baba yake mzazi kisa imani za kishirikina

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amewaambia wanahabari leo kuwa tukio hilo limetokea juzi saa moja jioni katika eneo hilo, ambapo marehemu alishambuliwa akiwa nje ya...

0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao

Mkazi wa Kijiji cha Upungu Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Jacob Mlela (88) ameuawa kwa kukatwa na shoka kichwani, shingoni na mikononi na mtoto wake Michael Jacob kwa kile kinachotajwa kuwa ni imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amewaambia wanahabari leo kuwa tukio hilo limetokea juzi saa moja jioni katika eneo hilo, ambapo marehemu alishambuliwa akiwa nje ya nyumba yake na kukimbizwa hospitali ya Ndalla lakini alifariki dunia 

Amesema chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina, kwani mtuhumiwa ana tatizo la kuanguka kifafa na mara kadhaa amekuwa akiamini kuwa baba yake ndio chanzo cha yeye kuugua ugonjwa huo.

“Mtoto anaugua ugonjwa wa kifafa ambao anaamini baba yake ndiyo chanzo cha yeye kuugua na kuchukua maamuzi hayo,” amesema.

Aidha Kamanda Abwao amesema mtuhumiwa huyo si tu kumuua baba yake bali pia alimjeruhi ndugu yake, Magdalena Jacob ambaye kwa sasa ana endelea vizuri akiwa anapata matibabu.

Kamanda Abwao ametoa wito kwa wananchi mkoa wa Tabora kutoendekeza imani za kishirikina na wanapokuwa wanaumwa waende kuwaona wataalamu katika Vituo vya kutokea huduma.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted