Msigwa:Serikali haijalipia kuweka tangazo la Tanzania kwenye jengo la Burj Khalifa. 

Msigwa amesema tangazo hilo la Tanzania linaonekana kuitangaza nchi hiyo limewekwa kutokana na uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu. 

0

Msemaji Mkuu wa Serikali, nchini Tanzania Gerson Msigwa amesema Serikali ya nchi hiyo haijalipia kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote duniani la Burj Khalifa, lililopo Dubai. 

Msigwa amesema tangazo hilo la Tanzania linaonekana kuitangaza nchi hiyo limewekwa kutokana na uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu. 

“Utawala wa Dubai umeweka tangazo hilo kwa kutambua ziara ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kaifanya Dubai na umeahidi kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia jengo hilo maarufu,”- amesema Msemaji huyo Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, kupitia ukurasa wake wa Twitter.  

Na kuongeza kuwa “Serikali haijalipia kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote Duniani liitwalo Burj Khalifa lililopo katika Jiji la Dubai. Tangazo hilo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu na Umoja wa Falme za Kiarabu”

Kauli ya Msigwa imekuja kufuatia taarifa mbalimbali zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu gharama kubwa za fedha zilizotumika kwenye tangazo hilo huko Dubai ambako kuna maonyesho ya DubaiExpo 2020, ambapo baadhi yao wamekosoa vikali juu ya matumizi hayo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted