Askofu Bagonza:Katiba Mpya ni msaada kwa watawala

Askofu Bagonza ameyasema hayo leo kwenye sherehe ya wanawake wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania chama cha CHADEMA, ambapo waliungana na wanawake wengine duniani katika kuadhimisha siku...

0

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt Benson Bagonza, amesema katiba mpya ni msaada mkubwa kwa watawala wa nchi hiyo kuliko ilivyo msaada kwa wananchi wa kawaida, huku akiwasihi  watawala waunge mkono jambo hilo.

Askofu Bagonza ameyasema hayo leo kwenye sherehe ya wanawake wa chama kikuu cha upinzania nchini Tanzania chama cha CHADEMA, ambapo waliungana na wanawake wengine duniani katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8.

“Katiba mpya ni msaada mkubwa kwa watawala kuliko ilivyo msaada kwa wananchi wa kawaida na nawasihi watala waunge mkono jambo hili” amesema Askofu Bagonza.

Askofu Bagonza ambaye ni kiongozi mkubwa wa dini nchini Tanzania mara kadhaa amekuwa akisikika kwa kuikosoa serikali iliyopo mamlakani kutokana na yale yanayoendelea nchini humo.

Mara nyingi amekuwa akiikosoa kwa kutumia falsafa za kisomi zaidi na kuwafanya baadhi ya watu kuchukua muda kumuelewa.

Hii leo Bagonza amesema “Utamaduni wa kutojali katiba una nguvu kuliko nguvu ya katiba mpya. Mazoea ya kutoheshimu katiba yana nguvu kuliko katiba mpya. Wanaovunja katiba mbovu tuliyonayo ndiyo haohao watakaovunja katiba mpya. Kibinadamu ni vema kuwa na katiba nzuri inayovunjwa na watawala wabaya, kuliko kuwa na katiba mbaya inayovunjwa na watala wabaya”

Nchini Tanzania kumekuwa na vuguvugu la madai katiba mpya kutokana na katiba ya sasa inayotumika nchini humo kutajwa kuwa ina mapungufu ya kisheria.

Hata hivyo vuguvugu hilo bado halijafua dafu, kutokana na kwamba utawala uliopo hauna ajenda ya kupatikana na kwa katiba mpya na badala yeke umesema katiba iliyopo sasa ya 1977 imejitosheleza.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted