Auawa baada ya kushambuliwa na Tembo hifadhi ya Ngorongoro

Kamanda wa Polisi MKoa wa Arusha ACP Justine Masejo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa limetokea Machi 9,2022 majira ya saa 7 mchana katika kijiji cha...

0
Kamanda wa Polisi MKoa wa Arusha, ACP Justine Masejo

Mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Narudwasha Titika (45), mkazi wa kijiji cha Alaitore kilichopo ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro amefariki dunia baada ya kushambuliwa na mnyama aina ya tembo sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda wa Polisi MKoa wa Arusha ACP Justine Masejo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa limetokea Machi 9,2022 majira ya saa 7 mchana katika kijiji cha Alaitore huko Ngorongoro.

Amesema uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa, marehemu alikutwa na mkasa huo wakati akitafuta kuni akiwa na wenzake ndani ya hifadhi ndipo alipo shambuliwa na tembo huyo. 

Baada ya kufanyika kwa uchunguzi mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi wanaoishi katika hifadhi, kuchukua tahadhari katika maeneo ya hifadhi za wanyama pori na kuhakikisha wanafuata maelekezo mbalimbali yanayotolewa na mamlaka za uhifadhi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted