Afisa wa Senegal asimamishwa kazi kwa matamshi yake juu ya wanawake na Uislamu

Rais alimuondoa Papa Amadou Sarr kutoka wadhifa wake wa uwaziri kama mjumbe mkuu katika shirika linaloitwa Fast-track Entrepreneurship for Women and Young People

0

Rais wa Senegal Macky Sall amemfuta kazi afisa mkuu ambaye katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake alikosoa mila za kienyeji za nchi na kuziita ‘upuuzi’ na kutamka matamshi mabaya dhidi ya wanawake kuhusu unyanyasaji wa wanawake — matamshi ambayo yalionekana kushambulia kanuni za Kiislamu.

Rais alimuondoa Papa Amadou Sarr kutoka wadhifa wake wa uwaziri kama mjumbe mkuu katika shirika linaloitwa Fast-track Entrepreneurship for Women and Young People (DER-FJ), taarifa ya serikali iliyotolewa Jumatano usiku ilisema.

Hakuna sababu iliyotolewa katika taarifa hiyo, lakini vyombo vya habari vya ndani vilisema alifutwa kazi kutokana na matamshi yake aliyoyatoa siku ya Jumanne kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Sarr alizungumza mbele ya kamera kwenye mkusanyiko wa wanaume na wanawake na maneno yake yalizua taharuki kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema hawezi kuelewa ni kwa jinsi gani katika karne ya 21 nchini Senegal “watu bado wanaweza kutamka matamshi ya kipuuzi kama,”mwanamke hawezi kusalimiana kwa mkono na mtu mtakatifu, na kwamba mwanamke hawezi kuwa katika chumba kimoja na mzee.”

Sarr alikiri kwamba alikuwa “anafanya mzaha” na akaendelea kuorodhesha ‘matatizo’ mengine yanayowakabili wanawake nchini Senegal, ambayo ni pamoja na kutoweza kufanya kazi au kulipwa mshahara mdogo kuliko mwanamume aliye na tajriba sawa.

Pia alizungumzia kesi ya mwanamke aliyeko kwenye hedhi kutoruhusiwa kuingia msikitini ‘mwanamke huyo huyo ‘mchafu’ anakupikia chakula chako na kulala kitandani kwako usiku.”

Maoni hayo yalitafsiriwa kuwa ni shambulio dhidi ya kanuni za Kiislamu katika taifa la Kiislamu.

Jamii ya Senegal ina sifa ya kuvumiliana. lakini mila na dini zinasalia kuwa mada nyeti.
DER-FJ inasaidia kufadhili na kusaidia uanzishaji wa biashara kwa vijana na wanawake.
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted