Watu 30 wauawa katika mashambulizi ya waasi mashariki mwa DR Congo

Mashambulizi hayo yalifanyika karibu na mpaka wa majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini

0

Takriban watu 30 wameuawa katika mashambulizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, afisa wa eneo hilo alisema Jumapili, huku kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF) likishukiwa kuhusika.

Kinos Kathuho, mkuu wa kikundi cha kiraia huko Mamove katika eneo lenye hali tete la Beni aliripoti vifo hivyo.

Alisema wapiganaji wa waasi wa ADF waliingia katika kijiji cha Mambumembume Ijumaa usiku.

“Kwa sasa, tuna idadi ya watu 27 waliouawa, nyumba kadhaa na pikipiki kuchomwa, watu kadhaa wamepotea,” alisema.

Makundi mengine mawili ya washambuliaji yalikwenda katika vijiji vingine viwili vya karibu, ambapo takriban watu watano pia waliuawa, aliongeza.

Kwa kuzingatia umbali wa eneo hilo na mawasiliano duni takwimu hizo hazikuweza kuthibitishwa.

Wakazi wa eneo hilo ‘wanakimbia kila upande’ alisema Kathuho, akiongeza kuwa ‘hakukuwa na jeshi’ katika eneo hilo.

Siku ya Ijumaa, kilomita 30 kutoka kwa mashambulizi hayo, raia watatu waliuawa katika mji wa Eringeti alisema Njiamoja Sabiti, afisa katika ofisi ya gavana wa NorthKivu.

Mashambulizi hayo yalifanyika karibu na mpaka wa majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini ambayo yote yamekuwa chini ya ‘hali ya kuzingirwa’ rasmi tangu Mei mwaka jana, katika jitihada za kuangamiza makundi yenye silaha ambayo yanakabili majimbo hayo mawili.

Chini yake, nyadhifa za juu za kiraia katika majimbo zimechukuliwa na askari wa jeshi au polisi.

Licha ya ukandamizaji — na usaidizi kutoka kwa vikosi vya Uganda, vilivyoanza kupambana na waasi hao mwishoni mwa Novemba – mashambulizi ya ADF yameendelea.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted