Balozi Polepole kupewa somo chuo cha Diplomasia kabla ya kwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Malawi.

Jana Machi 14, Rais Samia alimteua Polepole kuwa balozi ambaye anakwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Malawi, ambapo kabla ya nafasi alikuwa ni mbunge wa kuteuliwa na Rais.

0
Humphrey Polepole, Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani amemwambia Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole kuwa kabla ya kwenda kuanza majukumu yake ya kikazi nchini Malawi kama mwakilishi wa Tanzania, atatakiwa kwenda chuo cha diplomasia.

Rais Samia ameyasema hayo leo mara baada ya kuwaapisha Balozi Humphrey Polepole na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Kindaba, hafla ambayo imefanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

“Mh. Balozi najua baada ya hapa watakuweka darasani kwanza pale chuo cha Diplomasia, utakapotoka pale kabla hujaenda Malawi nitakutana nawe kwa hiyo tutazungumza kwa urefu”– Amesema Rais Samia Suluhu Hassani

Jana Machi 14, Rais Samia alimteua Polepole kuwa Balozi ambaye anakwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Malawi, ambapo kabla ya nafasi alikuwa ni mbunge wa kuteuliwa na Rais.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemtaka Balozi Polepole kwenda kuimarisha diplomasia kati ya Malawi na Tanzania kutokana na ukaribu ulipo baina ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo kuteuliwa kwa Humphrey Polepole katika wadhfa huo kumeibua hisia mseto kwa baadhi ya watu huku wengi wao wakisema kwamba huenda ikawa ndio njia ya kumfunga mdomo Polepole kutokana na ukosoaji aliokuwa akiuufanya tangu kuingia kwa Serikali ya Rais Samia.

Polepole alibadili upepo wake wa misimamo ya kisiasa na kimtazamo tangu tu ilipoingia madarakani Serikali ya awamu ya sita, tofauti na alivyokuwa na misimamo yake katika serikali ya awamu ya tano iliyokuwa chini ya Hayati Magufuli.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted