India imemkamata ‘daktari’ mlaghai aliyeoa wanawake 18

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 67 alivinjari tovuti za ndoa akijifanya kuwa daktari na kuwashawishi wanawake maprofesa, wanasheria, matabibu na afisa wa kijeshi kufunga ndoa naye

0

Bibhu Prakash Swain aliamini kuwa na rafiki wa moyoni na upendo wa kweli, ndivyo alivyowaambia angalau wanawake 18 aliodaiwa kuwaoa na kulaghai kote India kabla ya kukamatwa kwake — wiki chache kabla ya kufanya harusi nyingine mbili.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 67 alivinjari tovuti za ndoa akijifanya kuwa daktari mwenye umri wa miaka 51 na kuwashawishi wanawake maprofesa, wanasheria, matabibu na afisa wa kijeshi kote nchini kufunga ndoa naye, polisi walisema.

Nchini India ambako hadhi na cheo ni muhimu, alidai kuwa analipwa mshahara duni, na alitumia vitambulisho bandia na barua za miadi ili kuimarisha sifa zake na historia ya familia.

“Alifanya hivi kwa ajili ya pesa zao, na kushiriki nao ngono,” afisa mkuu wa polisi Sanjiv Satpathy aliiambia AFP.

Timu ya polisi Satpathy ilimkamata Swain katika siku za hivi majuzi baada ya miezi kadhaa ya uchunguzi wa harakati zake na akaunti za benki na mipango ya harusi mbili zilizopangiwa mnamo Februari na Machi.

“Alikuwa mshawishi sana,” Satpathy alisema, "na alilenga tu wanawake waliofaulu maishani na wasio na waume, wajane au walioachika walio katika umri wa miaka 40.”

“Siku chache za furaha na kuridhisha katika ndoa,” polisi walisema, Swain alikuwa akitoa visingizio vya kukopa pesa au vito vya wake wapya ili kumsaidia katika dharura.

Kisha akahamia kwa mwanamke mwingine aliyemlenga, akitumai kwamba hali za wanawake anaowalenga– kama mwanamke mseja, mjane au aliyetalikiwa na ambaye alikuwa ameolewa tena katika jamii ya kihafidhina — zingewatisha wasiende polisi.

Wachunguzi wanaamini kuwa Swain alioa zaidi ya mara 18 na sasa wanapitia rekodi zake za simu ambapo alihifadhi mawasiliano ya wake zake — kama Madam Delhi, Madam Assam au Madam UP (Uttar Pradesh) – wanawake walipewa majina ya maeneo walikotoka nchini India.

Wanawake wajawa na hasira kwa kudanganywa

Polisi walianzisha uchunguzi kuhusu maisha ya Swain mnamo Mei 2021 baada ya malalamiko ya mke mmoja mwenye umri wa miaka 48 ambaye, kwa bahati, aligundua kwamba tayari alikuwa ameoa angalau wanawake wengine saba.

Mwathiriwa, akiwa na hasira kwa kudanganywa, polisi wanasema, alipata mawasiliano ya wake wengine kutoka kwa simu ya mumewe na kuwasiliana nao kibinafsi kuhusu ulaghai wa muwe wao.

“Hapa ndipo tulipokuja na kugundua historia yake ndefu ya udanganyifu,” Satpathy alisema.

Swain, aliyezaliwa katika kijiji kidogo katika jimbo la mashariki la Odisha, alioa mara ya kwanza mwaka 1978 na ana watoto watatu — wawili wakiwa madaktari na mmoja daktari wa meno.

Akiwa amepata elimu kama fundi wa maabara, alikosana na familia yake na kuhamia mji mkuu wa jimbo la Bhubaneshwar ambako alianza kujitambulisha kama daktari na hatimaye akaoa daktari, mke wake wa pili, mwaka wa 2002.

“Tangu wakati huo ametumia majina mengi lakini kila mara alijitambulisha kama daktari au profesa huku akitafuta wake mtandaoni,” Satpathy alisema.

Polisi wanatilia shaka ujanja wake ulikuwa kazi ya mtu mmoja na wanatafuta watu ambao walimsaidia kwa mipangilio yake ya kina na kuhamisha pesa zake kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Gazeti la Hindustan Times lilimtaja kama mty mjanja, likisema alikuwa na kimo cha futi tano, urefu wa inchi mbili (mita 1.6), na kuripoti kwamba alioa angalau wanawake 27 katika majimbo 10.

Anadaiwa kulaghai benki 13 kati ya rupia milioni 10 (dola 135,000) na kadi za mkopo 128 za kughushi, na kuendesha mlolongo wa maabara ya matibabu ambapo madaktari na wafanyikazi wengine walikwenda kwa miezi bila malipo,gazeti hilo lilisema.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted