Tanzania kushiriki kikao cha Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa

Tanzania inashiriki katika kikao hicho ikiwa ni Mwenyekiti wa Nchi Wazalishaji wa Madini ya Almasi Afrika ( ADPA).

0

Waziri wa Madini nchini Tanzania, Dkt. Doto Biteko amekutana na Rais wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC), Bw. Collen Kelapile katika kikao kilicholenga kupata maelezo kabla ya kushiriki kikao cha Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika tarehe 18 Machi, 2022, katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.

Tanzania inashiriki katika kikao hicho ikiwa ni Mwenyekiti wa Nchi Wazalishaji wa Madini ya Almasi Afrika ( ADPA).

Aidha, kikao hicho kinalenga kujadili namna bora za kutumia rasilimali katika nchi husika kuibua maendeleo jumuishi kwenye jamii ambazo maliasili hizo zinapatikana ili zisaidie kuleta amani na hatimaye kufikiwa maendeleo endelevu.

Kikao hicho kitafanyika chini ya mada isemayo “Maliasili Jamii yenye Amani na Maendeleo Endelevu”

Wengine wanaoshiriki kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Madini wa Zimbabwe Wiston Chitando ambaye ni Makam Mwenyekiti wa ADPA, Mratibu wa Kimberly Afrika Bw. Jacob Thamage na Mwakilishi wa Kudumu Umoja wa Mataifa, Balozi Prof.Kennedy Gastorn.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted