Tanzania yafatilia uwapo wa aina mpya ya kirusi cha UVIKO-19.

Kirusi hicho, kinajumuisha kirusi cha Delta na Omicron, ambacho kimejiunda na kuwa kirusi kipya cha Omicron BA.1.

0
Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya nchini Tanzania , Ummy Mwalimu, amesema serikali ya nchi hiyo inafuatilia uwapo wa aina mpya ya kirusi cha UVIKO-19 kilichothibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Alisema kirusi hicho, kinajumuisha kirusi cha Delta na Omicron, ambacho kimejiunda na kuwa kirusi kipya cha Omicron BA.1.

Waziri Ummy aliyasema hayo jana jijini  Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungua mafunzo ya wataalamu wa upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na ugonjwa mahututi yanayofanyika katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Fahamu Muhimbili (MOI).

Alisema WHO inafanya utafiti wa kufahamu ukali wa kirusi hicho kipya na kwa upande wa wizara yake inaendelea kufanya utafiti kuwapo kwa kirusi hicho na kwamba ameshawaelekeza wataalam kufatilia suala hilo.

“Nimeshawaelekeza wataalamu wetu waangalie tuone kama kimeshaingia nchini kwetu kwa sababu nchi nyingine wameshathibitisha,” alisema Ummy.

Waziri Ummy aliwasihi Watanzania kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 ili kujikinga na kirusi hicho, kwani chanjo inasaidia pia kupunguza madhara ya ugonjwa huo

Hata hivyo hali ya uchanjaji bado ipo chini nchini humo kwa sababu asilimia 66 ya wanaougua UVIKO-19 waliolazwa hospitalini hawajapata chanjo, hali ambayo intajwa kuwa ni hatari kwa nchi 

Aidha Ummy alisema kama nchi nyingine ambazo kimeshatangazwa kuwapo, kuna uwezekano wa kuingia nchini kutokana na mwingiliano wa kibiashara katika mataifa mbalimbali duniani.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted