Tanzania imesema haifungamani na upande wowote katika mgogoro wa Ukraine na Urusi.

Balozi Mulamula amesema kwa miaka mingi sasa Tanzania inaamini katika kutafuta muafaka na maridhiano kwa kutumia njia ya diplomasia ili kumaliza migogoro.

0

Tanzania imesema haifungamani na upande wowote katika mgogoro unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine, na ndio maana ilipiga kura ya kutofungamana na upande wowote kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ametoa ufafanuzi huo kwa kusema kuwa  Sera ya Tanzania kuhusu namna ya kutatua changamoto za migogoro inapojitokeza ni kwa kutumia njia za kidiplomasia.

Balozi Mulamula amesema kwa miaka mingi sasa Tanzania inaamini katika kutafuta muafaka na maridhiano kwa kutumia njia ya diplomasia ili kumaliza migogoro.

Kutokana na muafaka na maridhiano kutopatikana katika mzozo wa Urusi na Ukraine, Waziri Mulamula anasema: “ndio maana katika kupiga tukaamua kutofungamana na upande wowote, lakini ilikuwa sio kutofungamana na pande zote mbili lakini ni kutoa ujumbekuonyesha kwamba sisi msimamo wetu na sera yetu na msingi wetu wa sera ya mambo ya nje ni kutokufungamana na pande zozote hasa katika hali kama hii”, alisema Mulamula.

Amesisitiza kuwa “Sisi msimamo wetu na Sera yetu na msingi wetu wa Sera yetu ya Mambo ya Nje ni kutofungamana na pande zozote, hivyo kutokupiga kura ni kuonesha msimamo wa Tanzania,” 

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tanzania imeathirika na mgogoro huo ikiwemo baadhi ya wanafunzi wa kitanzania waliokuwa wanasoma nchini Urusi kukatisha masomo yao na kurejea nchini wakisubiria vita kumalizika pamoja na ongezeko la bei ya petroli na gesi duniani.

Itakumbukwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizolazimika kuwaondoa raia wake nchini Ukraine hususani wanafunzi takribani 300 waliokuwa wakisomea masuala ya udaktari nchini humo.

Tanzania ilikua miongoni mwa mataifa 35 wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo hayakupiga kura kuunga wala kukataa azimio hilo lililoungwa mkono na mataifa 141, huku mataifa matano ya Urusi, Belarus, Syria, Korea Kaskazini na Eritrea, yakipinga azimio hilo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted