Vikongwe watatu wauawa kwa imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi mkoani Singida , Kamishna Msaidizi Stella Mutabihirwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea Machi 27, mwaka huu majira ya saa 11.00 jioni.

0

Ajuza watatu, wakazi wa kijiji cha Kisharita wilayani Iramba wameuawa kwa kuchomwa moto na wanakijiji wenzao kwa kile kinachodaiwa kuwa wamekuwa wakishiriki vitendo vya kishirikina.

Kamanda wa Polisi mkoani Singida , Kamishna Msaidizi Stella Mutabihirwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea Machi 27, mwaka huu majira ya saa 11.00 jioni.

Kamanda Mutabihirwa aliwataja waliouawa katika tukio hilo kuwa ni Agnes Msengi (84), Windila Saidi (80) na Winfrida Gigila (80) ambao wote kwa pamoja wanatuhumiwa kusababisha kifo cha Maria Enock ambaye alikufa Machi 26 kijijini hapo.

Kamanda Mutabihirwa alisema kufuatia tuhuma za wanakijiji na wanafamilia dhidi ya ajuza hao watatu, Mwenyekiti wa kijiji pamoja na Mtendaji wake walilazimika kuwachukua watuhumiwa na kwenda kuwafungia nyumbani kwa Mwenyekiti kwa mahojiano zaidi.

Alisema watuhumiwa hao walihojiwa kwa siku nzima hadi siku iliyofuata ambapo waliendelea kufungiwa kwenye nyumba hiyo wakati Mwenyekiti, Mtendaji wa kijiji na wanakijiji wengine walienda kumzika marehemu Maria.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted