Mashirika 19 ya Umma yapata hati zenye mashaka

CAG Kichere ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2021 kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali nchini Tanzania CAG Charlse Kichere

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali nchini Tanzania CAG Charlse Kichere, amesema taasisi 19 za umma nchini humo  kati ya 999 zilizofanyiwa ukaguzi kwa mwaka wa fedha 20220/21 zilikuwa na hati zenye mashaka.

CAG Kichere ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2021 kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Amesema katika mwaka 2020/21 amefanya kaguzi maalumu 56, kaguzi 37 zikiwa za mamlaka za Serikali za Mitaa, 12 Serikali kuu na sita mashirika ya umma na moja ya mifumo ya Tehama.

“Katika mwaka 2020/21 nimetoa jumla ya hati 999 za ukaguzi, kati ya hizo, hati 185 za mamlaka za Serikali za Mitaa, 195 mashirika ya umma, hati 308 serikali kuu, hati 19 vyama vya siasa, hati 292 miradi ya maendeleo,” amesema.

Kati ya hati 999 alizozitoa, hati zinazoridhisha ni 970, sawa na asilimia 97.1, hati zenye mashaka ni 19, sawa na asilimia 1.9, hati mbaya ni sita na nilitoa hati 4 za kushindwa kutoa maoni.

Amezitaja taasisi zilizopata hati zenye mashaka kuwa ni Jiji la zamani la Dar es Salaam, Halmashauri za Wilaya ya Kisarawe (Pwani), Longido (Arusha), Mlele (Rukwa), Musoma (Mara), Sengerema (Mwanza) na Bunda (Mara).

Kichere amesema kwa upande wa mashirika ya umma, taasisi zilizopata hati yenye mashaka ni Mamlaka ya Maji na Ustawi wa Mazingira Geita, Muleba, Ngara (Kagera), Tabora, Taasisi ya Mifupa Muhimbili na Mamlaka ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Nyingine ni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Amesema Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Reli Tanzania walishindwa kutoa maoni katika ukaguzi huo.

Aidha Kichere amevitaja vyama vya siasa ambavyo vimepata hati mbaya na zenye mashaka, ambavyo ni 

Chama cha CUF kimepata hati yenye mashaka ADC, Chaumma, UMD na TLP vilivyopata hati mbaya huku vyama vya CUF, UDP, SAU vikipata hati zenye mashaka.

Kichere amesema Chama cha Demokrasia Makini na AFP walishindwa kutoa maoni katika ukaguzi huo.

Hata hivyo amesema kuna ongezeko la hati safi kutoka asilimia 89 kwa mwaka jana hadi asilimia 98.01 mwaka 2020/2021.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted