Hatma ya Sabaya na wenzake kwenye kesi ya Uhujumu Uchumi kujulikana Mei 31

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo, ameitaja tarehe hiyo leo, na kwamba kwa kuwa watuhumiwa hao wapo mahabusu kesi hiyo itatajwa Aprili 13, 2022 kabla ya...

0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imepanga Mei 31, 2022 kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo, ameitaja tarehe hiyo leo, na kwamba kwa kuwa watuhumiwa hao wapo mahabusu kesi hiyo itatajwa Aprili 13, 2022 kabla ya kutolewa hukumu Mei 31.

Katika kesi hiyo mbali na Sabaya washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

“Mshitakiwa wa tatu ambaye hajasaini nampa siku moja kufanya hivyo, kesho awe amesaini na iletwe mahakamani. Kesi itatajwa Aprili 13, kwa sababu washitakiwa ni mahabusu na hukumu itatolewa Mei 31, 2022” amesema.

Hata hivyo Askari Magereza, Inspekta Ramadhan Misanga ameieleza mahakama kuwa Watson Mwahomange ambaye ni mshtakiwa wa tatu aliyekuwa akijitetea mwenyewe baada ya aliyekuwa wakili wake kujitoa, hajaweza kufika mahakamani hapo kwa sababu ni mgonjwa.

Aidha Hakimu Kisinda amemuongezea muda wa siku moja Mwahomange kuwasilisha hoja zake za majumuisho zikiwa zimesainiwa mahakamani hapo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted