Milipuko yatikisa Kyiv huku mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi yakiendelea
Msururu wa milipuko mikali ilitikisa maeneo ya makazi ya watu wa Kyiv mapema Jumanne na kuua watu wawili, saa chache kabla ya mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi kutarajiwa kuanza tena.