Kusaidia watu kufa ‘Euthanasia’ : Maeneo ambako ni halali barani Ulaya

Miaka 20 iliyopita, Aprili 1, 2002, Uholanzi ilikuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuhalalisha “euthanasia”, ambapo mtu husaidiwa kujitoa uhai.

0

Miaka 20 iliyopita, Aprili 1, 2002, Uholanzi ilikuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuhalalisha “euthanasia”, ambapo mtu husaidiwa kujitoa uhai.

Tangu wakati huo, barani Ulaya, ni nchi tatu tu ndizo zimefuata mkondo huo lakini zingine kadhaa zimepitisha sheria zinazowaruhusu watu wanaougua magonjwa yasiyotibika kujitoa uhai kwa kusaidiwa na wahudumu wa afya.

Wazo la kusaidia watu kufa bado lina utata mkubwa katika nchi za Kikatoliki kama vile Poland na Ireland.

Huu hapa muhtasari wa nchi za Ulaya zinazoruhusu watu kusaidiwa kujitoa uhai.

Nchi ambayo inarusu Kisheria kikamilifu: Uholanzi inaongoza

Mnamo 2002, Uholanzi ilihalalisha mpango wa euthanasia, ambapo madaktari humdunga sindano mgonjwa anayeugua ugonjwa usiotibika dozi ya dawa ambayo itamtoa uhai. Kabla mgonjwa hajadungwa dawa hiyo lazima madaktari wawili wakubali kuwa hali ya mgonjwa mahututi na hawezi kupata afueni na anateseka kwa maumivu makali.

Sheria ilisema kwamba wagonjwa walipaswa kuwa hoi.

Mnamo mwaka wa 2020, mahakama ya juu zaidi nchini iliamua kwamba madaktari wanaweza kutekeleza euthanasia kwa wagonjwa walio na shida ya akili bila kuogopa kushtakiwa, hata kama mgonjwa huyo hataonyesha wazi kuwa angependa kujitoa uhai.

Uholanzi pia ilikuwa ya kwanza duniani kuidhinisha euthanasia kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 12 na pia imesonga mbele kuelekea kuifanya iwe halali kwa watoto wagonjwa mahututi wenye umri wa kati ya mwaka mmoja na 12.

 Ubelgiji, Luxemburg, Uhispania zinafuatia

Ubelgiji ilikuwa inafuatia Uholanzi kwa karibu, ikiondoa vikwazo vya euthanasia mnamo Mei 2002 kwa wagonjwa wanaokabiliwa na mateso ya mara kwa mara, yasiyostahimilika na yasiyotibika ya kimwili au kisaikolojia.

Kwa wale wanaostahili kufanyiwa euthanasia ni lazima wawe na umri wa miaka 18 au zaidi na waombe kusitishwa kwa maisha kwa hiari, kwa hoja na kurudiwa-rudiwa, bila kulazimishwa na mtu yeyote.

Mnamo 2014, Ubelgiji ilikuwa nchi ya kwanza kuidhinisha watoto kuomba euthanasia ikiwa wanaugua ugonjwa usiotibika na ikiwa wao wenyewe wanaelewa matokeo ya kitendo hicho.

Katika nchi jirani ya Luxemburg, chapisho la kuhalalisha euthanasia katika baadhi ya matukio ya ugonjwa hatari yalipitishwa mwaka 2009. Haijumuishi watoto.

Uhispania ilijiunga na kundi hilo mnamo Juni mwaka jana, na sheria ya euthanasia kuruhusu wagonjwa mahututi au waliojeruhiwa vibaya kumaliza mateso yao kwa kujitoa uhai chini ya masharti.

 Kujiua kwa kusaidiwa

Uswizi inaruhusu kile kinachoitwa “kujiua kwa kusaidiwa,” ambapo wagonjwa hujidunga wenyewe dawa ambayo itawatoa uhai.

Hairuhusu daktari kumfanyia mgonjwa euthanasia lakini inaruhusu utoaji wa dawa ili kupunguza mateso, hata kama kifo ni matokeo ya mgonjwa kutumia dawa hizo.

Nchini Austria, sheria inayoidhinisha kujiua kwa kusaidiwa ilianza kutumika Januari 1, 2022. Hili lilikuja baada ya mahakama yake ya kikatiba kuamua kuwa nchi hiyo inakiuka haki za kimsingi kwa kuifanya kuwa haramu.

Mahakama ya kikatiba ya Italia mnamo Februari ilitupilia mbali ombi la kuitishwa kwa kura ya maoni juu ya kukomesha kujiua kwa kusaidiwa, ikiamua kwamba kura kama hiyo ingeshindwa kuwalinda walio dhaifu zaidi.

Mnamo mwaka wa 2019, mahakama ilikuwa imeamua kwamba mtu yeyote hapaswi kuadhibiwa iwapo atamsaidia mtu aliye na maumivu makali ya mwili au kisaikolojia kujiua.

Nchini Ureno, Rais Marcelo Rebelo de Sousa mwaka jana alipinga muswada ambao ungehalalisha ufikiaji wa usaidizi wa kujiua kwa wagonjwa wazima walio katika “mateso makubwa na maumivu makali na hawawezi kupona.

“Haki ya kufa”-

Nchini Ufaransa, sheria ya mwaka 2005 ilihalalisha euthanasia tu, ambapo mgonjwa ataondolewa mashine inayomsadidia kuwa hai, kama “haki ya kufa”.

Sheria ya 2016 inaruhusu madaktari kuhusisha hili na “kuwapa dawa wagonjwa ili wapoteze fahamu” hususan kwa wagonjwa mahututi, huku wakiweka euthanasia na usaidizi wa kujiua kuwa kinyume cha sheria hadi sasa.

Mswada wa sheria kuhusu euthanasia “ulio huru na kwa kuchaguwa” kwa wagonjwa wasiotibika nchini Ufaransa haukuweza kukamilika mnamo Aprili 2021.

Uingereza imeruhusu wahudumu wa afya kusitisha matibabu ya kuokoa maisha katika kesi tofauti tangu 2002.

Kufunguliwa mashtaka kwa wale ambao wamesaidia jamaa zao wa karibu kufa baada ya kueleza wazi nia ya kutaka kukatisha maisha yao imepungua tangu mwaka wa 2010.

Denmark imeruhusu watu kuwasilisha kwa maandishi kukataa matibabu ya kupita kiasi iwapo wanaougua magonjwa hatari tangu 1992, na hati hiyo ikihifadhiwa katika rejista kuu.

Euthanasia pia inaruhusiwa chini ya hali fulani nchini Ujerumani, Hungaria, Latvia, Lithuania, Norway na Uswidi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted