Bei ya Mafuta huenda ikaongezeka zaidi   

Chibulunje amesema soko la dunia la bei ya mafuta imepanda kwa kiasi kikubwa, ambapo kwa mwezi Desemba 2021 tani moja ya mafuta ya petroli ilikuwa inauzwa dola 717,...

0

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imesema kutokana na uhitaji mkubwa wa mafuta, bei ya bidhaa hiyo huenda ikaendelea kupanda bei zaidi hali inayochangiwa na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, huku usafirishaji na upokeaji wake nchini kuwa hafifu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Godfrey Chibulunje ameyasema hayo alipokuwa katika mdahalo uliohusisha Wahariri na waandishi wa habari hapo jana ambapo alisema kuwa, mfumuko wa bei unasababishwa na changamoto mbalimbali inayoikumbuka miundombinu ya usafirishaji kutokana  na sababu za kivita.

Chibulunje amesema soko la dunia la bei ya mafuta imepanda kwa kiasi kikubwa, ambapo kwa mwezi Desemba 2021 tani moja ya mafuta ya petroli ilikuwa inauzwa dola 717, na hadi kufikia Machi mwaka huu ilipanda hadi kufikia dola 1,106 kwa tani moja.

“Bei za mafuta zinatofautiana sana katika maeneo mbalimbali duniani, barani Afrika, Ulaya na Amerika, wakati Tanzania lita moja ya dizeli ikiwa inauzwa TZS 2,403, Kenya ni 2,331 na Uganda 2,830, hivyo ukiangalia nchini kulikuwa na unafuu kwa kiasi fulani,” amesema

Ameongeza kuwa April 5,2022 watatangaza bei mpya ya mafuta na mara baada ya vita kuisha hali itarudi kuwa shwari.

Pia aliwataka Watanzania kujiwekea utaratibu mzuri katika matumizi ya mafuta na kuangalia njia mbadala kama kuanza kufikifria kutumia magari yanayotumia gesi na umeme ili kuendesha shughuli zao.

Alisema kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya upokeaji wa mafuta bandarini ili kutatua changamoto zilizoko ndani ya uwezo wake na EWURA itaendelea kusimamia mwenendo wa uuzwaji wa mafuta hayo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted