Burkina Faso: Uamuzi wa kesi ya mauji ya Thomas Sankara kufanywa leo

Thomas Sankara alikuwa mkuu wa jeshi akiwa na umri wa miaka 33 tu alipoingia madarakani kwa mapinduzi mwaka wa 1983.

0
Thomas Sankara, Rais wa zamani wa Burkina Faso

Mahakama nchini Burkina Faso leo Jumatano inatarajiwa kutoa uamuzi uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu katika kuwashtaki wanaume 14 wanaotuhumiwa kumuua kiongozi wa mapinduzi Thomas Sankara, na kuhitimisha kesi iliyodumu kwa miezi sita na ambayo ilisimamishwa na mapinduzi ya kijeshi.

Akiwa anaheshimika miongoni mwa wafuasi wenye itikadi kali za pan-Africanist, Sankara alikuwa mkuu wa jeshi akiwa na umri wa miaka 33 tu alipoingia madarakani kwa mapinduzi mwaka wa 1983.Sankara alishambulia ubeberu na ukoloni, mara nyingi akiwakasirisha viongozi wa Magharibi lakini alipata wafuasi katika bara zima na kwingineko.

Yeye na wenzake 12 walipigwa risasi na kikosi cha washambuliaji mnamo Oktoba 15, 1987, kwenye mkutano wa Baraza la Mapinduzi la Taifa.

Mauaji hayo yalienda sambamba na mapinduzi yaliyomwondoa madarakani swahiba wa zamani wa Sankara, Blaise Compaore.

Katika kipindi chote cha utawala wake wa miaka 27, Compaore hakuweka wazi matukio yaliyopelekea kufariki kwa Sankara, na kuchochea uvumi kwamba yeye ndiye alikuwa mpangaji mkuu.

Kesi ya kihistoria kuhusu kifo cha Sankara ilifunguliwa Oktoba mwaka jana, zaidi ya miaka 34 baada ya kifo chake.

Washtakiwa bila kuwepo mahakamani

Waendesha mashtaka katika mahakama ya kijeshi katika mji mkuu wa Ouagadougou wamedai kifungo cha miaka 30 jela kwa Compaore, ambaye sasa anaishi uhamishoni katika nchi jirani ya Ivory Coast.

Compaore anashtakiwa bila kuwepo mahakamani kwa makosa ya kushambulia usalama wa serikali, kuficha maiti na kushiriki katika mauaji.

Anakanusha mashtaka

Upande wa mashtaka pia unapendekeza kifungo cha miaka 30 kwa Hyacinthe Kafando, ambaye anashukiwa kuongoza kikosi hicho.

Kafando, ambaye aliongoza walinzi wa rais wa Compaore, pia anashtakiwa bila kuwepo mahakamani.

Mhakama pia inataka kifungo cha miaka 20 kwa Gilbert Diendere, mmoja wa makamanda wa jeshi wakati wa mapinduzi ya 1987 na mshtakiwa mkuu aliyefika mahakamani kusikiliza kesi hiyo.

Tayari anatumikia kifungo cha miaka 20 kutokana na jaribio la mapinduzi ya kijeshi mwaka 2015. Katika taarifa yake ya mwisho, upande wa mashtaka ulisimulia kwa kina siku ambayo Sankara aliuawa.

Sankara alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa Baraza la Mapinduzi la Taifa, “wauaji wake walikuwa tayari washafika” ilisema.

Baada ya Sankara kuingia kwenye chumba cha mkutano, kikosi cha washambuliaji kiliingia na kuwaua walinzi wake, mwendesha mashtaka alisema.

“Kikosi kisha kiliamuru rais Sankara na wenzake kuondoka katika chumba hicho. Kisha wakawauawa mmoja baada ya mwingine.”

Wataalamu wa masuala ya risasi waliambia mahakama hiyo kuwa Sankara alipigwa risasi kifuani angalau mara saba na wauaji kwa kutumia risasi za kumimina.

Lakini washtakiwa walisema waathiriwa walikufa katika jaribio la kumkamata Sankara baada ya yeye na Compaore kutofautiana kuhusu mwelekeo wa mageuzi ya nchi.

“Kutaka haki”

Kesi hiyo ilisitishwa kwa muda baada ya mapinduzi ya Januari 24 ambayo yalimuondoa madarakani rais mteule, Roch Marc Christian Kabore.

Moja ya nchi maskini zaidi duniani, Burkina Faso ina historia ndefu ya machafuko ya kisiasa, lakini ilikuwa eneo la amani hadi waasi wa kijihadi walipovamia kutoka nchi jirani ya Mali mwaka 2015.

Machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu wapatao 2,000 na kuwafanya watu wapatao milioni 1.8 kuyahama makazi yao.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa tena baada ya mwanajeshi mpya Paul-Henri Sandaogo Damiba kurejesha katiba.

Compaore, ambaye aliondolewa madarakani na uasi mwaka 2014, amesusia kile ambacho mawakili wake wanakiita “kesi ya kisiasa.”

Prosper Farama, wakili anayeiwakilisha familia ya Sankara, alisema kuwa, kesi inapokaribia mwisho, familia hizo hatimaye zitapata ahueni — ingawa “wakati wa kesi hii, hakuna aliyekiri au kutubu. Hakuna hata mmoja!”

“Tunaomba mahakama izipe haki familia,” alisema.

“Hatutaki kulipiza kisasi, tunaomba haki tu.”

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted