Rihanna aingia kwenye orodha ya Forbes ya mabilionea

Nyota huyo ambaye anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake rapa ASAP Rocky, alitangazwa rasmi kuwa mwanamke tajiri zaidi katika muziki mwaka jana.

0
Rihanna, msanii na mfanyabiashara


 

Rihanna ameingia rasmi kwenye orodha ya mabilionea duniani, akiwa ameingia kwenye orodha ya kila mwaka ya Forbes kwa mara ya kwanza.

Utajiri wa nyota huyo wa Barbados unakadiriwa kufikia dola bilioni 1.7 unamweka kwenye nambari 1,729 kwenye orodha hiyo, ambayo inayojumuisha watu matajiri zaidi ulimwenguni.

Utajiri wake kwa kiasi kikubwa unatokana na ubia wake wa mitindo na vipodozi.

Kampuni yake ya vipodozi ya Fenty Beauty, ambayo anamiliki pamoja na muuzaji wa reja reja wa kifahari wa Kifaransa LVMH, iliipata mapato ya zaidi ya $550 milioni mwaka wa 2020, kulingana na Forbes.

Kampuni yake ya nguo za ndani ya Savage X Fenty, ambayo Rihanna anamiliki asilimia 30 ya hisa, ilikuwa na thamani ya $1bn mnamo Februari 2021.

Kujumuishwa kwa Rihanna kwenye orodha ya Forbes kumemfanya bilionea wa kwanza nchini mwao Barbados.

Nyota huyo ambaye anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake rapa ASAP Rocky, alitangazwa rasmi kuwa mwanamke tajiri zaidi katika muziki mwaka jana.

Katika mahojiano na The New York Times, alisema bado hajazoea hali yake mpya ya kifedha.

“Si rahisi kuzoea hali hii mpya ya maisha yangu kwa sababu najua nilikotoka,”alisema.

Kwingineko kwenye orodha hiyo, Kim Kardashian, Kanye West na Jay-Z wote pia wameorodheshwa kama matajiri wakubwa katika biashara ya burudani.

Kardashian alitangazwa rasmi kuwa bilionea mwaka jana, kutokana na biashara yake ya nguo za ndani ya Skims na ubia wake kwenye vipodozi. Ameorodheshwa katika nambari 1,645.

Mumewe wa zamani, Kanye West, ambaye sasa anafahamika kwa jina la Ye, ameorodheshwa kwenye nambari 1,513, akiwa na utajiri unaokadiriwa wa $2bn, alioupata kutokana na biashara yake ya viatu ya Yeezy na ubia wa muziki.

Jay-Z ameorodheshwa katika nambari 2,076, na wastani wa thamani ya $1.4bn.

Elon Musk alitangazwa rasmi kuwa mtu tajiri zaidi duniani.

Mwanzilishi wa Tesla na SpaceX, ambaye ndiyo kwanza amenunua hisa kubwa katika Twitter, ana wastani wa thamani ya $219bn.

Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, ambaye zamani alikuwa mtu tajiri zaidi duniani, alishuka hadi nafasi ya pili, ambapo sasa ana thamani ya $171bn.

Kwa jumla, mabilionea wapya 236 walijiunga na orodha hiyo, tofauti na mwaka jana ambapo mabilionea wapya 493 walitangazwa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted