Kombe la Dunia kufika Kenya katika ziara yake ya mataifa

Kwa mujibu wa sheria za Fifa, mbali na rais wa nchi, ni wachezaji waliokuwa sehemu ya timu iliyoshinda Kombe la Dunia pekee ndio wanaruhusa kushika kombe hilo.

0

Kombe la Dunia la Fifa litaletwa nchini Kenya Mei 26 na 27 katika ziara yake ya mataifa kadhaa duniani.

Debra Mallowah, Makamu wa Rais Coca Cola kanda ya Afrika Mashariki na Kati alisema Kenya ni miongoni mwa nchi chache za Afrika zilizochaguliwa kuwa mwenyeji wa kombe hilo kabla ya michuano hiyo.Kombe la Dunia la 2022 limeratibiwa kufanyika Novemba 21 hadi Desemba 18 nchini Qatar.

“Coca Cola imeshirikiana na kampuni ya Faifa kuleta kombe halisi la dunia la Fifa kwa ziara ya siku mbili nchini Kenya. Kenya ikiwa ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimechaguliwa kuandaa ziara ya kombe la dunia 2022,” alisema Mallowah.

“…Ninachukua fursa hii kuwaalika Wakenya wote kujumuika nasi katika kusherehekea kuwasili Mei 26 na 27.”

Kombe la Dunia la Fifa limetengenezwa kwa dhahabu ya karati 18 ikiwa na msingi wa madini ya malachite.

LIna urefu wa sentimita 36.8 na uzani wa kilo 6.1 na thamani yake ni KSh1 bilioni.

Kombe hilo litakuwa linakuja Kenya wakati Fifa imesimamisha nchi kutoka kwa shughuli zake zote kufuatia muingilio wa serikali.

Mnamo Novemba 11, 2021 serikali ilimtimua rais wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) Nick Mwendwa na maafisa wengine wa shirikisho hilo kwa madai ya ufisadi.

Miriam Limo, Meneja Mwandamizi Kenya alisema hivi karibuni watatangaza mahali ambapo kombe litaonyeshwa kwa umma.

Rais Uhuru Kenyatta pekee ndiye atakuwa na fursa nzuri ya kushikilia kombe hilo.

Kwa mujibu wa sheria za Fifa, mbali na rais wa nchi, ni wachezaji waliokuwa sehemu ya timu iliyoshinda Kombe la Dunia pekee ndio wanaruhusa kushika kombe hilo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted