Ripoti ya CAG yabaini uwepo wa dawa zilizokwisha muda wake kwenye hopsitali 15

Kwa mujibu wa CAG Kicehere hali hii inatokana na kupokea dawa kutoka kwa wafadhili na Bohari Kuu ya Dawa zenye muda mfupi wa matumizi

0

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania kwa mwaka 2020/2021 imebaini maduka ya dawa ya hospitali 15 za Rufaa na maalum nchini humo  yana dawa na vifaa tiba zenye thamani ya shilingi bilioni 1.63 ambazo muda wake wa matumizi umeisha. 

Ripoti hiyo iliyoishia tarehe 30 Juni 2021 ambayo iliwasilishwa na CAG Charles Kichere bungeni jijini Dodoma Aprili 12,2022.

Ripoti hiyo inaeleza, licha ya dawa hizo kuwemo hospitalini, uongozi wa hospitali hizo haujachukua hatua yoyote ya kuteketeza dawa hizo.

Kwa mujibu wa CAG Kicehere hali hii inatokana na kupokea dawa kutoka kwa wafadhili na Bohari Kuu ya Dawa zenye muda mfupi wa matumizi, kupungua kwa matumizi kutokana na kuanzishwa kwa dawa nyingine au mabadiliko ya mwongozo wa matumizi ya dawa zilizopo.

Amesema alibaini kuwa 34% ya dawa zilizokwisha muda wake ni kutoka hospitali Maalumu ya Kibong’oto zenye thamani ya shilingi milioni 552 ikifuatiwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi shilingi milioni 248, ikiwa ni 15%, hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bukoba shilingi milioni 221 ikiwa ni 14%, wakati hospitali nyingine za rufaa zinawakilishwa na shilingi milioni 608, sawa ni 37% ya dawa zilizoisha muda wake wa matumizi.

CAG amezitaja baadhi ya hospitali hizo zenye dawa zilizoisha muda wake ni, Amana, Temeke na Mwananyamala za (Dar es Salaam), Mbeya, Mbeya-Kanda, Songea, Singida, Dodoma, Tanga, Shinyanga, Tumbi (Pwani), Mount Meru (Arusha) na Hospitali Maalum ya Kibong’oto.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted